5,000 Tsh.

Bei

"Uchawi kila mahali upo japo serikali haiamini kuwa upo. Uchawi pia huleta utata kati ya raia na serikali. Raia wanaamini uchawi upo kwasababu unawakuta, serikali hawaamini kuwa uchawi upo kwasababu ya katiba pia wanaona kama usumbufu. Raia wengi wanaona uchawi kama ni mateso, kwa sababu ya kuteswa kwa kufanyishwa kazi pasipo kujijua kimazingara pia wanaona mateso kwa kurudishwa nyuma kimaendeleo. Kiasi kikubwa uchawi hauna nafasi serikalini tena hausikilizwi unaonekana ukakasi katika kazi. Siku zote uchawi unaogopwa na wanadamu pindi uonekanapo. Pia huwatishia amani na huwajenga hofu wanadamu. Uchawi hauna faida yoyote zaidi ya mateso na ufukara. Ijapokuwa wao wanaona kuna faida lakini hakuna chochote cha maana wanachokipata zaidi ya ufukara. Ukweli wanashangaza yaani mtu anatumikia uchawi toka utoto hadi uzee lakini mafanikio hana badala yake anaambulia fedheha. Mambo yote hayo ya nini ebu...tumpe Mungu nafasi ya kubariki maisha yetu. SONGA NAYO.... Mkoani Morogoro wilaya ya Mvomero kata ya Kibaoni kijiji cha Maharaka, anga yote ilionekana kutanda kuashilia mvua saa yoyote itanyesha. Hali ya hewa si shwari baridi lilikuwa kali kupita maelezo. Ardhi baada ya muda ikapoa ikaacha shamra shamra za wanakijiji zikilindima. Ndege nao walifurahia ujio wa mvua. Shorwe kwa makundi wakawa wanarukaruka

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Afisa wa jeshi la Magereza ASP James Nkongo, anaonesha ni mwenye hali ya kujitenga na aliyejaa chuki kwa maafisa wenzake na hata wafungwa. Huku akiongea na mkuu wa gereza pekee, ambaye anamheshimu kupitiliza. Siri nzito inajificha nyuma ya maisha yake, ambayo inajulikana na Mkuu wake sambamba na mfungwa mmojawapo hapo gerezani. Hakika ni huzuni na pia giza la moyo limeigubika nafsi yake.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Matunda ni aina ya kirutubisho muhimu, sehemu ya mlo kamili, ambayo ina sukari rahisi, yaani glukozi, pale itumikapo, moja kwa moja uingia ndani ya damu na kuanza kufanya kazi. Kadhalika, nafaka nzima, ni aina ya nafaka ambayo vile vitu vyote muhimu vitatu yaani, kiini, endospemu na ganda la nje vyote vipo na havijaondolewa kwa njia ya ukoboaji. Hivi vitu vitatu ndivyo vinavyohitajika na mwili wa mwanadamu kwa ajili ya kujilinda na maradhi, kurekebisha seli lakini pia katika ukuaji. Pale nafaka hii inapokobolewa, kitolewacho ni kiini na ganda la juu, inayobaki ni sehemu ya endospemu ambayo yenyewe huzalisha sukari nyingi iletayo maradhi mengi. Pia, mbogamboga ni sehemu ya mlo kamili ambayo ina umuhimu mkubwa sana katika kupatikana kwa vitamini ambavyo mwili hauwezi kuvizalisha na unavihitaji ili uweze kuwa na afya imara. Lakini pia madini muhimu kama chuma, magneziamu na fosforasi. Jambo kubwa la kuzingatia ni hili, hakika ni vyema tuwe na bustani majumbani kwetu, tupande haya makundi matatu, tuyakuze kwa samadi, yaani mbolea za wanyama nanjia

Sample Read

7,000 Tsh.

Bei

“Tuwa unataka niseme nini zaidi ya saluti?” “Ama kweli Hussein Tuwa unatukonga vilivyo,tunashukuru sana.” “Safi kaka! MTAFITI inatuliwaza sana. Pia inatusisimua.” “Dah! Hii riwaya kiukweli ni KUNTUU!” “I salute you, mkubwa. Hakika unaweza.” “Hii hadithi inaendelea kuwa nzuri kila siku! Kuikosa ni hatariiii!!!” “Jaman hadith hii kama isiishe vile, lakini ndo haiwezekani.Kaka unatisha. Nimeupenda sana mtiririko wa matukio BIG UP!” “Hakika kaka HUSENI TUWA riwaya zako ni nzuri sana natamani sana kukikamata kitabu cha hii riwaya ili nifaidi uhondo huu mwanzo mwisho.” “Duh, hii ni zaidi ya bongo movie kwa sababu hauwezi kutabiri next panatokea nini. Hongera sana Bradha.” “Bonge la movie! Ninaposoma utafikiri nipo ndani ya New world Cinema naangalia Movie...Thumbs Up, Bwana Tuwa.” “Unpredictable novel! BIG UP to the Author.” “Tuwa upo juu! Hii kazi imejaa ufundi wa hali ya juu sana. M/ mungu akuzidishie kaka!” “Haaa! Hussein Tuwa yaani wanimaliza ujue? You make me feel nipo Afrika kabisaaa! Yaani nakuvulia kofia.” “Nashukuru kwa kuipata kona ya riwaya reloaded kwani nilipoteza matumaini ya kuendelea na riwaya hii ya kusisimua na yenye mandhari halisi ya maisha yetu watanzania. Hongera sana mtunzi.” “Unanikumbusha sana enzi zile tukikusubiri uje kulala home kutoka Chuo, tupate mi-movie ya kusisimua.You were born to tell stories my brother!”-Kareem Tuwa “Kaka Tuwa unatambaa futi 70000 toka usawa wa bahari. Hii MTAFITI ni balaa tupu aisee. Thumbs Up, HT.” “Hili ni bonge moja la stori kaka. Kama vipi tuletee na kitabu chake kabisa, tupate kwenda sawa.” MTAFITI

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

“Ina maana unafurahia kwa ushindi wake?” “Of course yes! Jamaa anapiga ngumi za kilo nyingi, yaani kamtwanga Kibwana mpaka kamwacha na meno ishirini na nane…” “Na uhai kamwondoa!” “What? Unasemaje wewe?” “Ndiyo maana nikakuuliza unafurahia ushindi wake?” Badala ya kujibu swali lile Stella aliamua kuinuka na kutoka nje ya ukumbi huo uliosheheni watu waliokuwa wakishangilia kwa kelele na mbinja zenye kukera masikioni mwa wasiopenda. Ijapokuwa alipata upinzani mwingi kwenye katikati ya mashabiki hao wa mchezo wa ngumi, mwishowe alifanikiwa kutoka kabisa na kujikuta nje. Baada ya kujikuta nje akagundua kuwa hana pa kwenda zaidi ya kusimama na kushangaa magari yapitayo kutoka Kurasini kwenda Shule ya Uhuru. “Stella! Stella!” sauti ya kiume ikasikika nyuma yake ikiita kwa mbisho. Stella hakugeuka nyuma zaidi ya kuikusanya mikono yake kifuani mwake na kutulia kimya kabisa. Mtu mzima, ambaye ngozi ya mashavu yake tayari ilianza kujikusanya na kufanya makwinyanzi alisimama kando ya binti huyo. Hakuwa mtu mzima bali msichana mwenye kadiri ya miaka ishirini na tano na thelathini hivi. “Sasa kilichokutoa nje ni nini?” kule mtu mzima akauliza. “Sasa si pambano limeisha, nikae nifanye nini?” Stella akajibu. “Sidhani kama umetoka kwa sababu hiyo!” Yule mtu mzima akaonesha shaka. “Mzee taksi, twende!” dereva wa taksi alimwita mzee huyo kwa sauti kwa kuwa yeye alikuwa upande wa pili wa barabara ile. Gari yake aina ya Volvo ilikuwa bado inaunguruma. “Tuondoke na hii….” Yule mtu mzima akamwambia Stella. Msichana huyo hakujibu zaidi ya kubetua mabega ‘sitaki’. “Tunapanda UDA, sasa hivi litakuja…” “Utapandaje UDA na mimi nipo? We ni malkia wangu watakiwa kutumia kebu mama kufika kwako…”

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Kila mwanadamu aishiye chini ya jua hupenda kuishi maisha bora. Suala linakuja kuwa ni vipi atafanikiwa. Kila mmoja ana mbinu yake ya kutimiza ndoto yake kwa namna anayoona inafaa. Riwaya hii inagusa jamii tuliyonayo na iki chua yale yaliyotendeka miaka iliyopita na yanayoendelea kutendeka katika kipindi hiki. Songa nayo...

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa pesa ni zaidi ya kila kitu maishani. Ukiwa na pesa hakuna litakaloshindikana. Ni pesa hizo zinazoweza kuzua uhusiano mzuri kwa watu kama ambavyo pia zinavyoweza kusababisha maafa yasiyotarajiwa. Pesa ni sabuni ya roho na pia pesa huweza kuwa chachu ya matatizo. Katika riwaya hii ya aina yake, pesa zimedhihirisha jinsi zinavyoweza kuwa chanzo cha furaha maishani au kero na mtafuruku katika jamii. ni kipi kilichojiri? Fuatilia mkasa huu mzito wenye mchanganyiko wa mapenzi, visasi na mauaji ya kikatili...

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

ALIPOCHEKA, alipendeza. Tabasamu lake zuri, tabasamu linaloshawishi na kubembeleza, huwafanya watu, hususan wanawake wamsogelee na kumsalimia. Baadhi ya wanawake hao husisimkwa miili pindi tu waisikiapo sauti yake na huchanganyikiwa pale wanaposhikana mikono. Pia, alikuwa na sauti ya kipekee, sauti iliyogusa hisia zao na kuamsha gharika la maraha kwenye michipuo ya fahamu zao. Ni kijana wa kiume, mwenye sura ya ucheshi na macho ya upole. Hakuwa mwoga wa kutazamana na mtu, lakini hakupenda kutazamana na mwanamume mwenzake. Kwake, macho ya mwanamume mwenzake yalikuwa na kitu asichokijua, kitu kisichopendeza. Yalimtisha! Hata hivyo, hali hiyo ilikuwa kwa wanaume tu, siyo kwa macho ya wanawake. Aliyapenda macho ya wanawake na ilipotokea akakutanisha macho na kiumbe yeyote wa kike, katu hakuyabandua macho yake. Ndani ya mboni za mwanamke yeyote kulikuwa na kitu fulani kisichoelezeka, lakini kilichomvutia na kumsisimua.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Siyo kwamba kila mwanadamu anaamini kuwa ili utatute tatizo lolote linalokukabili lazima uwe na elimu ya kiwango kikubwa, uwe mjanja wa mjini au mcha mungu utegemeaye maombezi kwa kufanikisha mambo yako. Wapo ambao hawapo katika makundi yote hayo. Wao huamini zaidi katika kile kinachoitwa ‘nguvu za giza.’ Katika riwaya hii utashuhudia mambo yanayofanyika chini ya jua, yakiwastaajabisha wale wenye akili za kawaida na kuwasisimua wenye mioyo ya kijasiri.

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Ni asubuhi na mapema ndani ya mji wa Mafinga uliopo mkoani Iringa, Tanzania. Baridi likiwa kali sana. Watu walikuwa wanatembea mitaani huku wakiwa wamevaa makoti makubwa kupambana na baridi hiyo. Katika hoteli moja iliyopo katika mtaa wa Pipeline ndani ya mji huo kulikuwa na kikao cha siri cha watu wawili. Saa tatu sasa walikuwa wanapanga mikakati yao. "Sasa Martin fanya juu chini umpate Elizabeth Neville, ni yeye pekee ndio anajua kila kitu kuhusu mimi, na nina hakika endapo atathubutu tu kusema basi nimeangamia na ndoto yangu ya kuja kuwa rais wa Tanzania itakuwa imefikia kikomo." Lucas alisema kwa sauti ya upole na kusisitiza. "Usiwe na hofu yoyote Mheshimiwa Lucas. Mimi ndiye Martin, sijawahi kushindwa kazi yoyote ile. Ukiwa na tatizo lolote lile jua lifikapo kwa Martin limekwisha. Nipe siku tatu tu nitakuletea Elizabeth Neville mikononi mwako na utaamua mwenyewe nini cha kumfanya. Nakuhakikishia siri yako haitotoka katika mdomo wa Elizabeth Neville kwenda katika sikio lolote lile lingine hapa duniani." Martin alisema kwa kujiamini. "Nakuamini Martin Hisia. Sasa nakupa hizi milioni kumi za awali, na nitakupa milioni kumi na tano baada ya kukamilisha kazi hii. So milioni ishirini na tano ulizozihitaji zitakuwa zimekamilika" Lucas alisema huku akimkabidhi Martin bahasha yenye milioni kumi. Martin alizipokea, wakaagana. "Huyo Elizabeth Neville atakuwa anaijua siri gani ya waziri?. Maana kumpeleka kwake hiko kiumbe dhaifu tu katoa milioni ishirini na tano. Nitaifanya kazi hii siku mbili tu ili animalizie milioni zangu kumi na tano nilale mbele." Martin aliwaza akiwa ndani ya gari yake.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Walikuwa ni marafiki wenye kuelewana. Walikuwa ni marafiki wenye kushibana. Walikuwa ni marafiki unaoweza kuwaweka katika fungu la wakufa na kuzikana. Lakini pamoja na hayo yote, wawili hawa, hawakuwa marafiki walio kwenye kundi la wenye maumbile yenye kuendana. Na –kwa bahati mbaya- wala pia hawakuwa marafiki walio katika kundi la wenye tabia zenye kushabihiana. Na kubwa zaidi, na la kupendeza ni kwamba, marafiki hawa wote wawili walikuwa ni wasichana. Hiyo yoote ikiwa kama haitoshi, wasichana hawa wakatokea kuwa ni marafiki wenye majina yenye kufanana. Wasichana hawa kwa bahati, wakawa hawajatoka katika familia moja au familia zenye kufahamiana, lakini, wakadondokea katika ngekewa ya jina moja, kama vile wazazi wao walijua kwamba watakutana na kuwa kama mapacha. Mapacha ambao wako baba mbali mbali na mama kila mtu na wake. Mapacha ambao wataibuka na urafiki wa ajabu na wa kufurahisha, kuhuzunisha na kusikitisha, na hatimaye kufundisha. Marafiki hawa, wote wawili walikuwa wakiitwa Agnes, na kizuri ni kwamba, hata kifupisho cha majina yao kilikuwa kinafanana, kwani wote wawili walikuwa wakitumia kifupisho cha Agy.. Hawa wawili, walikuwa Agnes na Agnes.. Ama kwa kifupi unaweza kuwaita Agy na Agy.

Sample Read

1,500 Tsh.

Bei

Kitabu hiki ni kitabu kinachoelezea maisha ya Emmanuel Mathias, maarufu kama MC Pilipili. Kimeelezea maisha ya nguli huyu wa vichekesho nchini katika njia ya tofauti sana. Kitabu kina mahusiano ya moja kwa moja na vijana wanaliojikita katika sanaa na namna ya kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo. Msomaji wa kitabu hiki atapata funzo, hamasa na burudani kwa wakati mmoja. Katika sura ya kwanza ‘Asili Yangu’, msomaji atajifunza historia kupitia kitabu hiki ambapo mwandishi amewarejea Wagogo ambao ndiyo wahusika wakuu katika ‘Asili Yangu’.

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Mtoto Wa Kigogo ni simulizi ya kusisimua, iliyotungwa na kuhaririwa vyema na mtunzi Emmanuel Venance, ni simulizi ya mapenzi ya wapenzi wawili wapendanao ambao ni Binti mrembo Zabi kutoka familia ya kitajiri na Kijana mtanashati kutoka familia masikini Tom. Vikwazo na vitisho kwa wawili hawa hakikuwa kigezo cha wao kutengana wana simama imala na kulipigania penzi lao mwanzo mwisho. Hii ni Simulizi itakayokuburudisha, kukusisimua, na kukuelimisha pia lakini itakuacha ukiwa mwenye furaha na kamwe hautachoka kuirudia. Ungana na mtunzi ili upate uhondo kamili.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

UKUNGU MZITO UMEMTANDA kwenye jicho lake la kushoto. Anahisi jinsi lilivyovimba kutokana na uzito wa jicho lile pale usoni kwake akilinganisha na jicho lakejingine. Haoni vizuri. Mvumo mkali, unavuma masikioni mwake na kuzifanya kelele za watazamaji waliofurika ukumbini zisikike kana kwamba zinatokea ndani maji ya bwawa lililofurika... au kana kwamba yeye anazisikia kelele zile akiwa amezamishwa chini kabisa ya bwawa lenye kina kirefu. Hasikii vizuri. Kichwa kinamgonga. Sana, mfululizo. Kinamuwia uzito kuliko alivyopata kuhisi maishani mwake. Anakitikisa kwa nguvu na kututumua jicho lake moja linalofanya kazi kwa wakati ule ili aweze kuona vizuri. Anamuona mpinzani wake akitumia kamba za ulingo kujiinua kwa taabu kutoka kwenye sakafu ya ulingo ule waliokuwamo. Anainuka! Haamini hali ile. Hata baada ya kumtwanga ile ngumi ambayo huwa haimuachii mtu uwezo wa kuinuka tena? Kweli? Kweli. Mpinzani wake anafanikiwa kuinuka na kumgeukia akiwa ameinua mikono tayari kuendelea na pambano. Mwamuzi anamuwahi na kumzuia. Anamuuliza kitu huku akimuoneshea vidole viwili mbele ya uso wake. Mpinzani anatoa jibu. Mwamuzi anaonekana kuridhishwa na jibu lake. Yaani hata baada ya kichapo chote kile kilichoishia kwenye ile ngumi aliyoamini kuwa ndio ingemaliza pambano bado jamaa kaweza kuona vile ni vidole vingapi! Mambo mawili yanamfunukia kwa wakati mmoja akilini mwake. Kwanza anaona jinsi uso wa mpinzani wake ulivyochakaa kwa kipigo alichomshushia. Ulikuwa umetutumka kwa manundu. Macho yake yote mawili yalikuwa yamemvimba vibaya ilhali mdomo wake wa juu ukiwa umeumuka vilivyo, na kinywa chake kikiwa kimelowa damu. Pili anahisi ile sakafu iliyowambwa ya ule ulingo waliokuwamo ikiingia mabonde, naye anashindwa kusimama vizuri juu yake. Anayumba. Anamuona... kwa shida... mwamuzi akiziweka ngumi za mpinzani wake

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Mary alizaliwa nje ya ndoa, Bba Yake hakuwahi kumwona ingawa aliamini yuko hai. Alisikia baba Yake ni Mwarabu na Aliamini kwa sababu hata damu yake ilimdhihirishia ukweli huo. Alikuwa shombe wa kiarabu aliyezaliwa na mama wa kabila la kibondei mwenyeji wa Muheza mkoani Tanga. Hakuwahi kuambiwa jina la baba Yake, si kwa kutoka kwa mama Yake au babu yake aliyemlea. Lakini alisikia kutoka kwa majirani wakimtaja kwa jina la Mahfudh, jina ambalo lilipigwa marufuku kusikika kwenye familia Yake!. Alipewa jina la Mary kurithi jina la bibi Yake mzaa mama aliyefariki miaka mingi iliyopita. Akapewa ubini wa Goda ambalo ni jina la babu Yake, kwasababu ndiye aliyemlea. Akiwa bado Mdogo babu Yake anayemlea anafariki dunia. Anaanza maisha mapya kwa kulelewa na mama Yake mzazi. Kumbukumbu mbaya ya maisha Yake inaanza hapo... Riwaya hii inasisimua kuliko. Inaumiza kwa msomali na inakufanya uingiwe na jazba. -Kama ulikuwa jaujabahatika kusoma kitabu hiki kilichofanyiwa ukarabati mkubwa, kisome leo uone tofauti. Na kama ulikuwa haujawahi kusoma kitabu kilichoandikwa na BEKA MFAUME, anza na hiki, Lazima utatafuta kitabu chake kingine ~ Wasomaji.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Kundi kubwa la watu limeizunguka nyumba moja Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, mkoa wa Dar es salaam. Watu wamebeba silaha mbalimbali za kijadi wakiwa wamepandisha hasira sana, wakipiga kelele “Mtoeni huyo, mtoeni huyo, au tunachoma moto nyumba” mafuta ya petroli na viberiti vya gesi tayari vishakuwa mikononi mwao. Wapo waliotoka na Rungu, mapanga, sime, na visu pamoja na mikuki. Idadi yao kubwa wamebeba mawe. Kwenye nyumba ya jirani inayoendelea ujenzi wake, ndipo takrima ya mawe inapotolewa. Wanaokota mawe kila mmoja na jiwe analoweza kuliinua, analitwaa na kuingia katika mkumbo. Madereva wa Bodaboda nao hawakubaki nyuma katika sekeseke,

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Dereva Taxi Mwaduga Dingo, aliwapakia abiria asiowafahamu. Walipo ka mwisho wa safari yao, walikutana na askari wa doria. Wale abiria walikimbia, wakaliacha begi lao ndani ya gari ya Mwaduga Dingo! Askari walimzingira Mwaduga, wakamkamata, kisha walilifungua lile begi kuona kilichokuwa ndani, walikutana na silaha za kivita, bastola, na namba za gari bandia! Mwaduga anapelekwa Jela. Akiwa Jela anaiandika Barua ili iwa kie madereva Taxi wenzake. Kwa msaada wa msamaria mwema, barua ile ina kishwa kwa Inspekta Jamila. Barua ile inavumbua mambo mazito itakayokufanya ikuwache mdomo wazi. Inspekta Jamila anapoamua kufuatilia maelezo ya barua hiyo anahatarisha kazi yake na maisha yake Ili ajinasue inabidi aendelee kupeleleza, ndipo majanga, vifo, na hujuma asizozitarajia, anakumbana nazo! Sasa ikawa ni Mtego wa Panya. Hakika nchi na uchumi wake, ukawa katika matatizo mazito, yote kwa sababu ya BARUA KUTOKA JELA.

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Naitwa Dk. Barnabas Muzusa. Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya saba, na moja ya vitabu hivyo ni kile kiitwacho, “GHARAMA ZA UONGOZI”. Wewe Mkazi yeyote katika nchi yoyote ulimwenguni nakushauri usome kitabu hiki cha UCHUMI kilicho andikwa na Mwalimu mjasiriamali, Ndugu ARAM JAPHETH KAYENGELA; Ambapo baada ya kukisoma na kukipitia nimegundua kwamba, kitakupa hekima kubwa kuhusu namna unavyoweza kuinua uchumi wako katika nchi mbali mbali za Afrika, ulaya, marekani, na penginepo. Zaidi naweza kusema kwamba, kitakusaidia kujua namna ya kufungua kampuni, kujipanga kiuchumi na kuwa na akiba wakati wa uzee. Wengi wameandika kuhusu haya, lakini naona huyu Mwalimu mjasiriamali, amechambua pointi nzuri kabisa na za muhimu sana. Kumbuka kwamba, kuinuka kwa uchumi wako ni pale ambapo uchumi wako unapokuwa na uwezo wa kukupatia mahitaji yako, na kuwagusa watu mbali mbali wanaokuzunguka. Kwa muhtasari huu ninaweza kuwashauri watu wote ulimwenguni kutokuruhusu kabisa hata wazo dogo; linaloweza kuujengea utashi wako ukuta wa kutokukitaka kitabu hiki cha uchumi. Kwa hiyo ninapendekeza kukipitisha kitabu hiki kuwa moja ya vitabu bora kabisa duniani; na ninawaalika wote kukisoma. Asanteni .

Sample Read

7,000 Tsh.

Bei

Ni miaka mitatu tangu kuuawa kwa Osama bin Laden nchini Pakistani. Wanamgambo wa Al-Qaida walikuwa wamesambaratika. Wengi miongoni mwao wakiwa wameuawa, ilhali wengine wakikamatwa na majeshi ya Marekani nchini Pakistani... na kikundi cha wachache wengine kikiwa kimefanikiwa kutoroka na kukimbilia eneo la Waziristani lililo kaskazini mwa Pakistani, kwenye kitongoji cha Miramshah kilichokuwa kinadhibitiwa na washirika wao wakuu, wapiganaji wa Taleban. Huko wakapata hifadhi baada ya kifo kile kichungu cha kiongozi wao. Na tangu wakati huo, hali ya wakaazi wa kijiji kilichokuwa kiasi cha kilomita saba kutoka kwenye ile ngome ya watalebani iliyowahifadhi wale wanamgambo wachache wa Al-Qaida, imekuwa ni ya mashaka makubwa. Njaa ilikuwa imetawala, mahitaji yote muhimu yakatoweka, maradhi hayakuwa na wa kuyatibu, magonjwa ya mlipuko na yatokanayo na lishe duni yakishamiri...

Sample Read

4,000 Tsh.

Bei

Wakati dunia ikihaha kutokana na upungufu wa ajira duniani, hali inabadilika ghafla na kuwafanya wasomi kukosa jibu kwa elimu zao. Hapa ndipo vyeti vinavyodhibitisha elimu za wasomi hawa toka kila kona ya dunia kuwa ni bure kabisa. Ugunduzi wa vifaa maalumu vya kurahisisha kazi maofisini, vikiwepo computer na maroboti ya kila aina ndio sababu ya kukwama kwa ajira nyingi. Sio jambo la kificho tena kuwa wasomi kutoka vyuo vikuu na vile vya kati wapo kwenye changamoto ya aina yake. Lakini kwa upande mwingine Ujasiriamali umekuwa ndilo jibu pekee na suluhisho la uchumi duniani. Dunia sasa inapokea watu wenye nguvu ya vipaji kuwa sehemu ya uponyaji wa uchumi. Kwa hakika Ujasiriamali ndilo jibu hasa kwa dunia ya leo. Ndani ya kitabu hiki kuna mengi yaliyoainishwa ili kutoa njia ya namna ya kuuponya uchumi wako. Fursa ziko nyingi za kukufanya uhesabiwe kuwa bilioni baada ya miaka michache. Mafanikio ya nayopatikana kwenye ujasiriamali ni tofauti sana na yale yanayopatikana kwenye ajira ya mwajiriwa. Utajiri wa mjasiriamali hauna maswali wala hisia za kifisadi! Hili ndilo jibu pekee sana kwa kila mtubila kujalisha amesoma ama la. Kwa mengi ya thamani kubwa karibu ndani ya kurasa za kitabu hiki cha aina yake.

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Nilizaliwa tarehe 02/02/1978 katika kijiji cha ujamaa Nambalapala kilichopo Kata ya Kipara, Zone ya Mnero Mission, Tarafa ya Ruponda wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Mkoa huu ni maarufu sana kwa kupatikana kwa gesi asilia pia kulima zao la korosho, mandhari yake haitofautiani sana na visiwa vya Zanzbar. Wenyeji wengi wakiwa waumini wa dini ya kiislamu. Nikiwa ni mzaliwa wa pili kati ya watoto nane kwa wazazi wangu, mzee Abdalah Mohamed Musa Maigala na mama yangu kipenzi Asumin Hamisi. Wazazi wangu walikuwa wakulima huku wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama yalivyo maisha ya kijijini. Maisha hayakuwa mazuri sana na kutokana na kipato kidogo, hivyo tulilazimika kukomaa kimawazo tukiwa katika umri mdogo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Nilikuwa mdadisi sana kuhusiana na mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea katika familia yetu tangu nikiwa mtoto. Nakumbuka siku moja niliwauliza wazazi wangu namna ambavyo nilizaliwa mpaka nakua. Mama alishangazwa na swali langu akainamisha kichwa chake chini kisha akavuta pumzi na kusema; “Mwanangu Suleiman sasa umekua, nasema hivyo kwa sababu swali ulilouliza linaonyesha kuwa unataka kujitegemea kiakili” Baada ya kusema maneno hayo alivuta tena punzi na kunitazama huku akitokwa na machozi kisha akaendelea; “Wewe ni mtoto wangu wa pili. Ilikuwa usiku wa manane nilipoanza kuhisi uchungu, Baba yako alichukua baiskeli yake na kufunga tenga lake la kwendea shambani ili nikae humo. Mwanangu ilikuwa hakuna jinsi ya kupata usafiri mwingine kwa nyakati hizo za usiku. Nilipata taabu kubwa sana njiani kwa sababu tenga lile nililobebewa lililkuwa dogo hivyo kunipa wakati mgumu katika ukaaji.

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Kamba Kiroboto yuko katika ulimwengu wa aina yake. Katika kipindi fulani maishani alijiona kuwa yu binadamu kamili, mwenye heshima mbele ya jamii, kwa watu wa marika yote. Halafu kikaja kipindi ambacho alijiona hatofautiani na mnyama. Akajenga chuki dhidi ya wanadamu wenzake, hata akakaribia kujenga chuki dhidi ya nafsi yake. Hali hiyo haikutokea kama muujiza, hapana. Kulikuwa na sababu maalum. Ndipo anapoweka nadhiri ambayo hakuwa tayari kuitengua kwa namna yoyote ile. Anaamua kufanya chochote kile, wakati wowote, mahali popote na dhidi ya mtu yeyote mlengwa. Huenda hicho atakachokifanya kikawa kizuri kwake lakini kikawa ni pigo zito kwa mwingine. Hata hivyo, hajali athari yoyote itakayotokea upande wa pili. Ana msimamo thabiti katika uamuzi wake. Kama atakuwa amevunja sheria ya nchi hilo ni jambo lingine, lakini ameamua. Uamuzi wake ndiyo kitu muhimu hata kama utekelezaji utaigharimu roho yake... anajiamini na anaamini kuwa uamuzi wake ni sahihi zaidi ya ushauri wa mwanadamu mwingine yeyote aliyezaliwa chini ya jua. Vitabu vingine vitakavyotoka hivi karibuni ni MILIONI THELATHINI, KARATA YA BARADHULI na GUBERI LA KIMANYEMA. Kitabu kingine ambacho kiko sokoni ni DOMO LA MAMBA.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Wakati niki kiria kuchapa kitabu cha riwaya hii, mmoja wa wasomaji wangu ambaye aliwahi kuisoma gazetini, aliniambia kuwa ilimvutia sana na hivyo, akawa akiisubiri kwa hamu. Hata hivyo, mchakato wa uchapaji ulikumbwa na matatizo yaliyosababisha kusitishwa kwa muda uchapaji. Zilipopita siku nyingi, msomaji huyo, Clara John aliniuliza ni kwa nini sijakichapa kitabu na aka kia hatua ya kuwa tayari kugharimia uchapaji huo. Nikiwa katika maendeleo ya kuufanyia marekebisho mswada huu, mara mawasiliano kati yangu na Clara John yalipotea. Nikajitahidi kutafuta kwa njia ya mtandao wa Facebook na WhatsApp, sikumpata. Simu yake pia ikawa haipatikani hewani. Ni baada ya takriban mwezi mmoja baada ya kupoteza mawasiliano ndipo nilipopata taarifa kuwa alifariki dunia gha a kwa presha akiwa huko mkoani Iringa. Ilikuwa ni taarifa iliyonisikitisha sana kwani tayari nilikuwa katika hatua za mwisho za kwenda kiwandani. Nguvu ziliniisha, nikajikuta nikikata tamaa na kutojisikia hamu tena ya kuuchapa mswada huu. Jambo lingine lililonichaganya ni kuhusu picha yake iliyokuwa imeandaliwa kama pambo la jalada, jambo alilolia ki. Sikuwa najisikia kuwa radhi kuitumia tena ilhali yeye mwenyewe hayupo duniani. Ingependeza kama angelikuwa hai, akishike kitabu chenye jalada lenye picha yake! Hata hivyo, baada ya kujadiliana na baadhi ya watu wake wa karibu, nikashauriwa niitumie tu picha yake katika kumuenzi. Tulimpenda Clara John, lakini Mungu alimpenda zaidi.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Shabaan Gerebwa au Gerry Money alikuwa ni kijana chotara aliyechanganya rangi ya Mataifa mawili kati ya Tanzania kwa mama na Ujerumani kwa upande wa baba, tangia utoto wake Gerry hakuwa na rekodi nzuri ambayo unaweza kusema ilichafuka mapema tangia akiwa tumboni kwa mama yake ukubwani akiwa mbaya zaidi kwa maana ingekua jambo jepesi kukutana na simba mwenye njaa kali kuliko kukutana na chokoraa huyo mweupe na kubaki hai, kwa maana kitu kuua kwake halikuwa tukio la kustaabisha kabisa na mbaya zaidi ni pale alipokutana na rafiki yake wa utotoni Aisha ama kwa jina la umaarufu Lady Madudu, mwanamke chakaramu ambaye licha ya kumiliki genge kubwa la uhalifu pia alikuwa ni bosi wa danguro akidiriki hata kuuza madawa ya kulevya bila ya woga wowote kutokana na kuwa na mtandao mkubwa uliohusisha hata askari wasio waaminifu kwa Taifa lao, sheshe zaidi liliibuka pale jeshi tiifu la Polisi lililipotia mkono wake kati na kusababisha ulipuke moto ambao haukuwa rahisi kuzimika kwa maji ya kidebe........

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Lucy aligonga mlango na kuingia moja kwa moja hadi ndani bila kusubiri kukaribishwa. Alipokwishaingia, ndipo macho yake yalipiga kwenye sofa moja kubwa ambapo aliwaona Teddy na Eddy. Teddy aliendelea kusoma kitabu kilichokuwa mikononi mwake huku amejilaza kifuani pa Eddy, ambaye alikuwa akimchezea nywele zake kwa mkono mmoja ilhali ule mwingine ukiendelea kubadili idhaa za runinga kwa rimoti. “Jamani wenyewe humu ndani,” Lucy alisema baada ya kukutanisha macho na Eddy aliyekuwa ameugeuzia uso wake mlangoni kufuatia mchakato wa miguu, “Hamjambo?” Eddy hapendezwi na kasumba ya Lucy kuingia ndani bila kukaribishwa, walakini alizi cha hisia zake; ghadhabu zilibaki moyoni, uungwana akauvaa usoni. Pamesemwa kwamba muungwana hanuni usoni. Eddy alimjibu, “Oh, Lucy!”

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Maswahiba wawili wanaodhaniwa wamefanana tabia, mmoja wao anahukumiwa kifungo cha Miaka arobaini jela kwa wizi wa mamilioni ya shilingi. Anatumikia kifungo hicho kwa miaka ishirini na mitano. Kifungo chake kinabadilisha kila kitu nyuma yake. Mwenzake, maisha yake yanabadilika. Umiliki wa pesa hizo unamwezesha kuwa na Uchumi Mkubwa. Anakuwa mfanyabiashara maarufu anayemiliki casino kubwa inayomwingizia mamilioni ya pesa. Anajenga himaya kubwa na kumweka karibu na viongozi wa juu wa mamlaka za dola serekalini. Anamiliki mtandao mpana wenye kuogopwa. Anajijengea heshima kubwa, anaogopwa na hagusiki! Anaitwa, mzee Beka! Mwenzake anayitwa Ben Kamanyola anatoka jela! Anakumbana na msimba wa kumpoteza kipenzi mama yake mzazi na dada yake waliopenda sana. Anagundua nyuma ya vifo hivyo kuna mkono wa swahiba huyo! tofauti zinajitokeza kati ayo. Mzee Beka anatumia nguvu yake kiuchumi kummaliza rafiki yake, lakini anagundua uwezo mkubwa wa akili aalionao swahiba weke ni kikwazo kinachompa wakati mgumu kupambana naye! Mlipuko unaotokea kati yao, ni sawa na Nyaya mbili za umeme positive na negative zilizogusana! Duh, sijawahi kusoma riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa kiufundi kama hii, Inazuhuzunisha, inakujengea hofu, inakutia woga na inakuingiza kwenye vita vyao! Hutakubali kruka hata senigs moja. Hapa ni kurasa moja baad aya nyingine. Hulali! ~ Maundu Mwiingizi, Author Ukitaka kuujua ugiwji wa Beka Mfaume, isome riwaya hii, Utajua ninachoamaamanisha! - Innocent Ndayanse. Mwandishi na mhakiki wa riwaya mbalimbali.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Mary alizaliwa nje ya ndoa, Bba Yake hakuwahi kumwona ingawa aliamini yuko hai. Alisikia baba Yake ni Mwarabu na Aliamini kwa sababu hata damu yake ilimdhihirishia ukweli huo. Alikuwa shombe wa kiarabu aliyezaliwa na mama wa kabila la kibondei mwenyeji wa Muheza mkoani Tanga. Hakuwahi kuambiwa jina la baba Yake, si kwa kutoka kwa mama Yake au babu yake aliyemlea. Lakini alisikia kutoka kwa majirani wakimtaja kwa jina la Mahfudh, jina ambalo lilipigwa marufuku kusikika kwenye familia Yake!. Alipewa jina la Mary kurithi jina la bibi Yake mzaa mama aliyefariki miaka mingi iliyopita. Akapewa ubini wa Goda ambalo ni jina la babu Yake, kwasababu ndiye aliyemlea. Akiwa bado Mdogo babu Yake anayemlea anafariki dunia. Anaanza maisha mapya kwa kulelewa na mama Yake mzazi. Kumbukumbu mbaya ya maisha Yake inaanza hapo... Riwaya hii inasisimua kuliko. Inaumiza kwa msomali na inakufanya uingiwe na jazba. -Kama ulikuwa jaujabahatika kusoma kitabu hiki kilichofanyiwa ukarabati mkubwa, kisome leo uone tofauti. Na kama ulikuwa haujawahi kusoma kitabu kilichoandikwa na BEKA MFAUME, anza na hiki, Lazima utatafuta kitabu chake kingine ~ Wasomaji.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Sam Kisogo anaanzisha uhusiano na mwanamke mrembo ambaye pia ni mke wa mtu, anayeitwa Cathy, Uhusiano huo unakuwa wa siri. Tatizo linakuja pale siri hiyo inapogundulika... Mauaji yanatokea, ushahidi unamlenga Sam Kisogo. Mwenyewe anaapa siye aliyeua. Mtu pekee anayemuamini Sam hakuua ni Cathy. Swali, ni nani atakayethibitishia Mahakama kuu Sam siye muuaji? -Soma kitabu hiki upambane na riwaya iliyoandikwa kiufundi. -Ni haki yake kuiitwa The greatest !

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Wivu wa mapenzi ni eneo lenye mtihani mkubwa kwa binadamu, hauchagui elimu ya mtu, akili ya mtu, kipato cha mtu, jinsia au wajihi wa mtu, humwingia yeyote mwenye kupenda. Hugharimu maisha yako na ya yule umpendae, hula gharika na sumu yake humtafuna mtu akiingia hai! Wivu wa mapenzi huikoroga akili na kukugeuza kuwa mwendawazimu pale unapohisi kuna mtu anachangia ndani ya penzi lako. Wivu huumiza, unatia hasira na kukufanya ufanye maamuzi ya hove na kukuleta majuto baadae huku yakikufanya uyaone maisha yako hayana thamani!. Penzi ni wivu, bila wivu hakuna penzi! Hapo ndipo mgogoro unapoanzia... Futatana na mwandishi mahiri Beka Mfaume kwenye riwaya hii ya aina yake ya mapenzi hasa kama sasa hivi upo ndani ya penzi. -Riwaya hii inamfanya Beka Mfaume sio tu mwandishi mwenye kipaji cha akin Yake, lakini pia ni gwiji anayejua nini maana ya mapenzi -Gazeti la visa. -Mara ya kwanza nilipoisoma riwaya ya MWIBA nilijikuta nikiapa kuwa, Beka Mfaume hatoweza kuandika riwaya nyingine kali ya mapenzi yenye msisimko wa kipekee kama MWIBA. Leo hii Beka Mfaume ananidhihirishia nilikuwa nimejidanganya kuwaza hivyo!. Isome riwaya hii kama ilivyo ya MWIBA zingechezwa filamu! Mohammed Kuyunga, Global Publishers.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Dodoso la riwaya UMASIKINI wa kutupwa unamfanya Suma Kiroba a kirie mara mbili namna kuogelea kwenye utajiri. Ni jambo gumu mno kwake waka akiwa hana kianzio chochote. Hana elimu. Hana fedha wala kipaji cha sanaa yoyote! Hana chochote. Ni fukara wa kutupwa akibangaiza kuingiza siku kwa kufanya vibarua. Hata hivyo, siku moja anapata wazo. Stori za mitaani kuhusu uhusiano mwema wa majini na binadamu na namna unavyowatajirisha zinamvu a. Suma anatamani kuingia kwenye mapenzi na jini ili aweze kutajirika. Kwake, ilikuwa bora kuwa na uhusiano na jini ili awe tajiri kuliko kuoa binadamu ambaye angemtegemea na kumzidishia shida! Sekeseke linaanzia hapo. Suma anasaka mbinu za kuwavu a majini na kufanikiwa. Jini mrembo anaingia mikononi mwake na kuyabadilisha kabisa maisha yake. Raha ya utajiri inageuka simulizi yenye matukio ya ku sha na kusisimua. Kila kitu kilikuwa sawa... ta zo lilikuwa moja tu. Mashar ndani ya mkataba wa kupewa utajiri. Usipoteze muda, anza kusoma ufaidi mwenyewe...

Sample Read

2,500 Tsh.

Bei

Dume Suruali ni mwanaume wa aina gani? Tafsiri yake ilikuwa na uzito zaidi kama Brian angeielezea sababu ndiye aliyempa Kevin jina hilo. Kwanini lakini? Ni kwasababu kwa nafasi aliyokuwa nayo na fedha tele alizozikusanya zilimpa kiburi cha kumchezea mke wa Kevin, Prisca vyovyote alivyotaka na Kevin alijua kila kitu. Mke wa mtu ni simu, lakini vipi kama sumu hiyo ikimpata mke mwenyewe? Kevin atakubali kuendelea kuwa Dume Suruali milele?

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

SIRI YA RAIS ni mfululizo wa riwaya inayoyaakisi maisha ya muuguzi, Tamali. Akiwa binti mbichi, maisha yake yanaingia mashakani. Mateso anayoyapata Tamali na mama yake yanatokana na siri nzito aliyoamua kuitunza kwa kuulinda wajihi wa baba yake kisiasa. Baba yake ambaye ni Rais Patrick Mzobe anachukua jukumu la kumkalia kooni bintiye ili asipate nafasi ya kuuanika uovu ambao taifa lilistahili kuujua. Je, ni siri gani Tamali anaificha na kuyafanya maisha yake yawe ya mashaka dhidi ya baba yake? Inaanza hivi…. KWA NINI? Kwa nini dunia ni onevu sana? Kwa nini ni sahaulifu? Si sahaulifu tu, bali haitendi haki kwa uonevu na kiburi. Haki ya kila mja mwenye pumzi na mapenzi ya kuishi vile atakavyo haipo duniani. Mwenye haki na kiu ya kuyafanya maisha yake yawe yake, peke yake pasipo vikwazo wala uonevu, akiwasaidia wengine kwa huba, hugeuka mhanga. Siwezi jua kwa undani. Siwezi amini kama kweli macho yangu ni makengeza, ubongo wangu umechoka kufikiri, hata sauti yangu haitoki nje ya jumba hili la mateso. Inawezekana, sauti yangu kufungiwa na mawazo yangu kuchacha kisha kuangamia ndani ya jumba hili la wahalifu? Je, ni makusudi ya aliye niumba. Tazama, ukuta mrefu umelizunguka jumba hili na kulinyima hewa ya kutosha. Tupo ndani ya shimo kama si pango la wanyonge. Mbali na kuta zake ndefu, senyenge yenye moto, imetanda kwa hila. Yote hayo asitokee mtoro, mtoro muuaji, mtoro mtoa roho. Najiuliza, je, mimi kweli ni muuaji? Hapana! Mie sijaua. Sijawahi kuua hata kuwaza kuutoa uhai wa kiumbe yeyote duniani kwa jeuri. Kazi yangu ni kuyafanya maisha ya kila kiumbe yastawi kama mche wa ua waridi kwenye udongo mzuri. Maisha ya kila kiumbe ni matamu awapo huru kuiona nuru, akitumbukizwa katikati ya giza la uvungu maisha yake huwa ya mashaka kama popo asiyeweza kujitafutia mchana. Nakumbuka kisha nasahau, sijui hapa nilifika lini na nitatoka lini. Nasikia mkisema kwa sauti za kunilaani, “Kaa mbali na Tamali katili, kwake kuua ni jambo rahisi kama kuubeba unyoya wa kuku.” Nawasikia lakini siwezi kuwajibu. Siwashangai wala siwapuuzi, hiyo ni nafasi yenu na uhuru wenu kwa sasa. Haya ni maisha yangu nisiyo yaota wala kuyawaza kuishi nayo tangu kuzaliwa kwangu. Ningali nikiendelea kuwaza, nimedhoofu mwili wangu, nipo hohehahe sijiwezi. Nunua na pakua riwaya hii uburudike na kuelimika…

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Mpaka Edo akiwa anakata simu, bado Lilian alikuwa hajaitoa simu yake sikioni. Edo akapotea machoni mwake alipoingia tu kwenye chumba cha ukaguzi. Bado Lilian hakutaka kuondoka. Aliendelea kusubiri pale uwanjani hadi nusu saa baadaye. Kila ndege iliyokuwa ikianza kuruka uwanjani pale na Lilian kuiona, aliishia kupunga mkono. Vyovyote itakavyokuwa, yeye aliamini kati ya ndege hizo, mojawapo mpenzi wake Edo angekuwa ndani yake. Ndicho kitu kilichokuwa akilini mwake. Bahati mbaya sana kwake ni kwamba, kati ya ndege hizo alizokuwa akizipungia mkono, hapakuwa na hata moja ambayo ndani yake alikuwepo Edo. Lilian aliondoka uwanjani pale akiwa mwenye huzuni sana. Bado Edo alikuwa akilini mwake, ilikuwa vigumu sana kumtoa kichwani mwake. Edo alikuwa kila kitu katika maisha yake. Miaka miwili iliendelea kujirudia kichwani mwake. Haikuwa rahisi kusubiri kwa muda wote huo, lakini moyoni aliamini angeweza maana alijua kushikilia msimamo wake sawasawa! SASA ANZA KUBURUDIKA MWENYEWE...

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Vijana wawili wanapendana hatimaye kuzama kwenye msitu mnene wa mahaba. Miaka minane inakatika wakiwa kama ndizi kwenye mkungu wake wakipeana kwa hamu. Siku inatokea msichana anawaza hatma ya mapenzi yao pasipo ndoa, anaamua kumuuliza mpenziwe juu ya kutaka kumfanya mkewe………anajibiwa kwa swali ambalo lilizaa jina la riwaya hii..”Kwa nini nikuoe wewe?” Baada ya swali hilo, mambo yanageuka na kuwa kindumbwendumbwe, kulikoni!!! ONJA KIDOGO MAZUNGUMZO YAO HAPA Kwa nini niliamua kumvulia nguo Rich wakati si mume wangu? Akiniacha je, itakuwaje? Hapana, ni vema nichukue hatua. Miaka minane ni mingi sana hasa ukizingatia wanaume maarufu kama huyu ni majanga matupu. Leo anaweza kuwa na mimi, kesho na mwingine na keshokutwa pia. Ananiwazia nini mtu huyu. Je ananipenda kama vile nampenda? Hapana, lazima niujue ukweli leo pasipo kificho.” Ha! Rose alijikuta akijawa na hamu ya kuuliza swali. Alitaka kujua hatma ya uhusino wao huo wenye furaha. Haya, Rose anauvunja ukimya hapa; Rose: Richard! Dear! (Alimtikisa) Rich: Hey! Vipi mpenzi! Rose: Amka bwana. Umelewa? Rich: Acha uzushi bwana. Nilewe nini tena? Nimepumzika tu mpenzi. Huoni leo ni faragha yetu kushinda zote? Huna budi kufanya hivyo, tulale. Rose: Kuna jambo nataka tulizungumze mpenzi. Nyanyuka basi nikueleze!(Wakati huo, Rose alimshika mkono Richard kumnyanyua na wote waliketi kitandani. Rose alimwegemea Richard kifuani huku mkono wake ukizichezea sharafa zake. Wakati hajaongea lolote, Rose alishikwa na kigugumizi). Rich alilianzisha; Rich: Mh! Nieleze basi dear, nini kinakusibu? Rose: Ah-m! Anyway, Rich- kuna jambo nataka kukueleza! Rich: Ok! Endelea! Rose: Nimezungukwa na furaha mwili wangu wote kwa ajili yako. Umeyafanya maisha yangu yawe na furaha hadi leo. Nina jambo naomba nikuulize mpenzi. Please, usi…………Mh! Rich: Mbona unahofu. Ongea…….. “you are free” (“uko huru”) Speak anything (ongea chochote) Rose: Sawa dear. Nina swali nataka nikuulize. (Wakati huo Rose alikuwa aking’atang’ata vidole vyake kwa aibu. Kisha aliendelea….)
….Richard! sasa ni miaka minane imepita tangu tuwe wapenzi. Kati yetu, sote tumekuwa na furaha isiyo mfano na inatufanya tufurahie mapenzi yetu (Alishusha pumzi)---A’h-m!........Napenda kufahamu mpenzi, lengo lako ni lipi juu ya mapenzi yetu? Kikubwa zaidi…………….A-mm! Basi Rich: Vipi tena? Wewe ongea usihofu chochote hapa. Hujanizoea tu miaka yote hii? Rose: Si hivyo Rich. Utanioa lini niwe mkeo wa ndoa mpenzi? Nahisi umri pia muda mwingi umepita hatulizungumzii hili! Samahani lakini. Rich: (alinyamaza kimya akimtazana Rose usoni kwa makini. Alishusha pumzi na kisha aliuliza swali baada ya Rose kumaliza kuongea kwake) Naomba tafadhali nieleze, nani kakutuma uniulize swali hilo? Tumeishi muda wote bila kuniuliza swali kama hilo. Vipi, unaweza kunieleza, ni nani amekutuma uniulize? Umepata bwana aliyekudanganya kukuoa nini? Haya niambie nijue nijikate ingali mapema sijachelewa.  Rose: Samahani Rich. Sikupanga iwe hivyo lakini……….Ah! Rich: Lakini nini? Sikiliza Rose, nakupenda sana zaidi ya unavyodhani. Lakini ninahitaji na wewe unijibu, uko tayari? Rose: Ndiyo Rich, please! (tafadhali) Rich: Ok!.....Sasa fahamu kuwa, sitakuoa wewe Rose. Unaweza kunieleza, kwa nini nikuoe wewe? Baada ya jibu pia swali lake Richard, Rose alibaki kimya akimkodolea macho huku akitokwa na machozi. Hakika furaha yake iligeuka uchungu mkali ulioiteka nafsi yake. Aliwaza na kuwazua mengi wakati huo. Aliwaza pengine ingekuwa sahihi kwake kumuadhibu Richard vikali. Kama si hivyo, alihisi pengine bora angejiua kuikwepa aibu. Upande mwingine wa nafsi yake ulimtaka avute subira pengine amjibu Richard swali lake kuwa kwa nini anastahili kuoana naye. Yote aliyatafakari akiwa mkimya na bumbuwazi lilimshika. Alitamka pasipo hiari yake kwa hasira kisha alinyanyuka. “SAWA! SAWA Rich! Hakika ngoja nikuonyeshe” Alinyanyuka na kutoka kitandani kwa jazba. Je, nini kilifuata kati yao?

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Hatua za maisha ya msichana hufanana sana na maisha ya Kipepeo aishiye na kukua katikati ya wadudu au viumbe wenye hila. Adui mkubwa wa Kipepeo anajitokeza, huyu ni Kinyonga aliyejificha ndani ya maua mazuri. Je, Kipepeo ataweza kuzitimiza ndoto zake katikati ya VINYONGA wenye njaa na kiu ya kumtafuna? Mfululizo wa riwaya hii unayamulika maisha ya kila msichana aishiye katika uso wa Dunia. Sehemu hii ya kwanza ambayo ni HAMANIKO inayaangaza maisha ya msichana LOLA, binti wa Majaliwa mwenye ndoto za lukuki. Kwa hila anabakwa siku ya mkesha wa Noeli baada ya kutiliwa dawa za kulevya kwenye soda. Baadaye Lola anashika ujauzito kisha jamii inamkataa na kumtenga kwa upofu wa sheria za kijiji chake. Hamaniko linamjaa moyoni, hamjui baba wa ujauzito aliokuwa pia hofu ya ndoto zake kumpotea. Lola hafi moyo anapambana kuyaunga maisha yake yaliyo chakaa. Je, Lola atapata nafasi ya kuyaungaunga maisha yake yaliyochakaa kama cheni na kuzitimiza ndoto zake pasipo kikwazo? Usiache kufuatilia mfululizo wa kisa hiki cha kusisimua na kuelimisha.

Sample Read

1,500 Tsh.

Bei

Simani ni mtoto pekee katika familia yao. Anaishi na mama yake katika kijiji cha Ngirikisande. Maisha yao yamegubikwa na umaskini uliokithiri baada ya baba yake kupotea katika mazingira ya kutatanisha (wakati Simani akiwa mtoto mchanga) alipoenda kuwinda kwenye pori la Mtevyamajini linalohofiwa kuwa na majini yalayo watu. Simani anafichwa siri hiyo hadi anapokuja kuifahamu akiwa na miaka kumi na mbili. Akiwa amechoshwa na maisha ya kutokuwa na baba na kutaniwa na marafiki zake kijijini hapo, Simani na mbwa wake Boji wanatoroka na kufunga safari ya kwenda kumsaka baba yake kwenye pori la Mtevyamajini, lenye majini hatari.

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

KIU YA DAMU -FADHAA ni riwaya ambayo msuko wake ni wa kisimulizi. Riwaya hii inasimulia kisa cha kusisimua ambacho kiliikumba familia moja huko Bagamoyo. Kijana Mbununu anafumwa na kiu ya kuimwaga damu ya mkewe wa ndoa aliyekuwa mjamzito, kwa wivu wa mapenzi alihisi mkewe huligawa tunda lake la huba kwa jirani yake. Hisia za kisasi zinamfanya Mbununu kuua mfululizo kisha anajaribu kujiua ili kuukwepa mkono wa sheria. Kabla hajafanikiwa kujiua, Mbununu anaokolewa na jeshi la polisi kisha kupelekwa hospitalini ambako anapata tiba kisha kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma zilizomkabili. Jambo la kushangaza, Mbununu asiyejua kusoma wala kuandika, anaipoteza sauti yake kutokana na dawa zilizolikwangua koromeo lake. Je, mahakama ilichukua hatua gani kuujua ukweli wakati Mbununu hakuwa akijua kusoma wala kuandika, pia hakuwa na sauti tena ya kuweza kujieleza kwa kina? Soma ndani ya riwaya hii ujifunze jinsi mkasa huu unavyoweza kuyabadili maisha yako ya kila siku.

Sample Read

4,000 Tsh.

Bei

NAJUA WA KUMPA ni riwaya ambayo inauweka wazi udhalimu ambao mtoto wa kike hukumbana nao ndani ya jamii nyingi za Kiafrika. Msichana Semeni anapambana kuupinga mfumo huo kandamizi kwa kumpinga baba yake ambaye anataka bintiye aolewe kwa nguvu na mtoto wa rafiki yake ili kuulinda uhusiano unaohusu biashara haramu.

Je, Semeni akiwa msichana ambaye jamii inamhisi kuwa dhaifu atafanikiwa kumshinda nia baba yake ambaye ana uchu wa mali kwa kumtumia mwanaye kama chambo?

TATU KIONDO ni mwandishi na mtunzi chipukizi wa riwaya za kiswahili, anao weledi na upeo pia juhudi za kutosha kuifanya kalamu yake kuisemea jamii nzima inayomzunguka. Ni mwandishi ambaye kazi zake zina
ujazo wa maarifa na lugha ya kuvutia. 
Riwaya hii ni sahihi kwako kuisoma ili ujue ukweli wa mambo yaliyomo ndani.

Sample Read

4,000 Tsh.

Bei

Muhtasari kidogo: St. Augustine University of Tanzania, 2008 Nenda rudi ya hapa na pale ilitawala eneo la chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kilichopo jijini Mwanza. Ilikuwa ni asubuhi iliyojaa kila aina ya pilikapilika, wapo walioonekana wakikatiza huku na kule wakiwa katika mwendo wa haraka, wapo waliokuwa wamesimama vikundi vikundi wakiendeleza mijadala ya hapa na pale. Wapo walionekana kujikunyata kwenye viti vilivyokuwa eneo maarufu la kupumzikia lililojulikana kama Mapanki wakijisomea na wengine wakipiga soga ili mradi kila mmoja alikuwa na namna yake na kuvuta muda ili kuufikia wakati muafaka wa kuingia madarasani. Hali ya ubaridi asubuhi hii ilifanya wanafunzi wengi wawe ndani ya makoti na masweta huku wengine wakijitanda mitandio mizito kuipunguza ile baridi. .....

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Kimo anajikuta njia panda, kuufuata moyo wake au kumridhisha baba yake. Anaamua kucheza kamari ya maisha kwa kwenda kinyume na kile baba yake alitaka awe. Anajikuta akifukuzwa nyumbani kwao na kumlazimu kuanza maisha ya ghetto, ambayo hajawahi kuyapitia. Kwenye maisha ya upangaji anakutana na Munerah, anayependana naye lakini penzi lao halidumu baada ya Munerah kulazimishwa kuolewa Oman. Wanaachana wakiwa bado wanapendana sana. Kimo anakutana na Jamillah, msichana maarufu na mrembo kupita kiasi aliyekuwa akimpenda mno hadi kubandika picha zake ukutani. Anajikuta akipigania vitu viwili vikubwa, kutafuta mafanikio kumthibitishia baba yake kuwa kwa kufuata moyo yake hakuwa anapotea na kuliwinda penzi la Jamillah, msichana wa ndoto yake mikononi mwa Branx.

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Mike, kijana dereva taxi jijini Dar es Salaam, anambeba mteja wake wa kike, Natasha kumpeleka kwenye miadi yake usiku wa manene. Anajikuta akiwa sehemu isiyo sahihi kwa muda usio sahihi. Wanakabiliwa na hatari dhidi ya askari wa cartel kubwa Afrika Mashariki, Paka Weusi, wauza dawa za kulevya wenye hila. Wanatiwa nguvuni kisha kutupwa kwenye ‘Handaki la Kifo’, jela maalum kwa waasi wa kundi hilo. Wakati akiomboleza kifo cha kinyama cha mpenzi wake, Natasha, anakabiliwa na kazi mbili kubwa – kulipiza kisasi cha kuuliwa kwa mpenzi wake na kujinasua kutoka sehemu ile hatari hatari zaidi chini ya ardhi, sehemu ambayo hakuna aliyewahi kutoka hai. Je, Natasha atafanikiwa kulishinda jeshi hatari la Red Poison, mwenye miliki ya vyombo vya sheria na silaha

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Mapenzi huponya mapenzi huangamiza kuwa makini. G aka Ganzi, kijana katili muuaji asiye na chembe ya huruma, anadondoka katika penzi zito la msichana mrembo aitwaye Tausi. Miezi mitt kabla, kajan hutu alikuwa hahitaji kuta na Rafiki wala mpenzi, akiongoza operesheni za kijambazi za kundi maarufu na katili liitwalo Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, lakini baada ya kutokea mrembo huyo, anajikuta akiwa amezama hasikii haoni kwa mrembo kiasi cha kujikuta akiamua kusaliti kundi hilo lililomlea na kumtajirisha na kuamua kumwaga damu ya yeyote anayetaka kumtenganisha na mrembo Tausi. Lakini kumbe asilolijua ni kwamba… Riwaya hii iliwahi kutamba sana katika magazeti ya Jangwani, Kiu na Jambo leo kiasi ambacho mwandishi alipata maoni hayo, sasa uhondo upo muelle ya macho yako. Nakuhakikishia, utakapokishika kitabu hiki na kuanza kukisoma hutatamani kukiweka chini mpaka ukimalize na huenda baada ya kukimaliza ukaamua kurudia kukisoma tena na tena…

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Kuandika riwaya ili ichapwe gazetini ni jambo moja. Kuandaa muswada wa riwaya kwa madhumuni ya kuchapwa kitabu ni jambo jingine. Domo la Mamba ni riwaya ambayo niliitumia katika gazeti moja na kupata simu nyingi zinazoulizia kitabu chake. Wengi niliwajibu. Baadhi yao waliridhika kwa majibu yangu, baadhi hawakuridhika. Niligundua kuwa wasomaji wengi hu kiri kuwa gharama za uchapaji kitabu hazizidi shilingi 500 kwa nakala moja. Mtu mmoja alidiriki kuniuliza: “Shilingi laki tatu au nne hazitoshi kuchapa nakala elfu moja au mbili?” Nilishangaa, nikakosa jibu! Gharama za uchapaji zimepanda maradufu. Ukitaka kuchapa kitabu chenye zaidi ya kurasa 100 itabidi ujipange na kujikamua mifuko na hasa kama unataka kitabu hicho kiwe kwenye ubora unaostahili. Isitoshe, linapokuja suala la kuandaa muswada inabidi baadhi ya mambo yafanyike, miongoni mwa yaliyo muhimu yakiwa ni uhariri na uhakiki. Haya nayo hugharimu pesa zisizo haba. Kitabu hiki nimekiandaa katika mazingira magumu lakini nikiwajali zaidi wasomaji wangu na jamii kwa jumla. Ni katika kipindi hicho ndipo nilipowagundua mara ki wa kweli, walioijua dhamira yangu huku pia wakitambua ka jinsi mtikisiko wa uchumi ulivyoniteteresha katika kuitimiza azma yangu. Ni mara ki hao ambao walikuwa nami bega kwa bega, wakiniunga mkono kwa hali na mali, tendo lililochangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uchapwaji wa kitabu hiki. Ninawashukuru sana ndugu na mara ki hao na zaidi, ninawashukuru wasomaji wangu ambao mara nyingi wamekuwa wakinihimiza kuchapa vitabu vya riwaya nilizotoa katika magazeti mbalimbali. Domo la Mamba ni mwanzo wa matoleo ya riwaya hizo. Nyingine ziko jikoni, zikiiva, zitapakuliwa na kutengwa mezani tayari kwa kuliwa. Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

MESEJI ZA SIMU KUHUSU MDUNGUAJI KUTOKA KWA BAADHI YA WASOMAJI WAKATI RIWAYA HII ILIPOTAKA KWA MARA YA KWANZA KWENYE GAZETI LA KIU YA JIBU MWAKA 2006: “Duuh! Hii ni baab kubwa mzee mwenyewe. Hadi tunaunguza mboga kwa kusoma Mdunguaji! Endelea kutupa uhondo huu adimu nchini.Big Up Tuwa.” “Big Up sana mtu wangu, THE SNIPER ni mfuniko mnene. Imebana vilivyo na nategemea uhondo zaidi.” “Tremendous pressure, even to the very best! Wape akina Sword sh, Honey B na Stealth relief kidogo Mr. Tuwa!” “Mambo vipi bro? Mzee unatisha MDUNGUAJI imenishika vibaya sana! Big Up! Keep it Up!” “Hi! Babu kama vipi tuandalie kitabu, THE SNIPER ni noma mzee. Tumekukubali.” “Tuwa nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa riwaya zako lakini MDUNGUAJI imevunja rekodi. Kweli una kiri sana na una uwezo mkubwa wa kujenga visa sisimuzi.” “Mambo yako yatakuwa sa . Sisi wapenzi wa riwaya zako tunaomba THE SNIPER uitolee kitabu.” “Ebwana mtu wangu unazidi kunidatisha na riwaya yako ya THE SNIPER. Mwana mi bado nipo nawe, vipi kitabu lini?” “Baba naikubali hii riwaya yako (Mdunguaji).Maoni yangu kabla haijakwisha tupate kitabu.” “Bw. Tuwa nadhani ukitoa tuzo kwa wasomaji bora, na imani nami nitakuwa mmoja wao, hivyo ushauri wangu na THE SNIPER iweke kwenye kitabu tupate uhondo kwa pamoja, au tunga vitabu tu mbona tushakukubali na tunajua kuwa we ndio bingwa kwa riwaya zinazosisimua nchini?” “Ebwana mambo vipi mzee Tuwa? Mwanzo ulikuwa unanichanganya lakini sasa unanipa ile kitu roho inapenda. (THE SNIPER) inatisha. Kaza buti mzazi,tuko pamoja.” “Hussein Tuwa sina ushauri wala maoni isipokuwa kukupongeza kwa kipaji chako. Hongera sana man. Mimi ni mwanajeshi. Namfagilia sana Baddi Gobbos, natamani kuwa kama yeye.”

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Riwaya hii imejumuisha sehemu zote mbili za kisa hiki, yaani PART 1 na PART 2 kwa pamoja, kinyume na namna kilivyotoka kwenye kitabu kigumu ambapo vilitoka vitabu viwili tofauti kila kimoja kikiuzwa elfu 8. Sasa hapa unapata kisa cha vitabu vyote viwili kwa elfu 8 tu

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

MAONI YA BAADHI YA WASOMAJI KUHUSU “KIBWE KATIKA SAFARI YA AJABU” BAADA YA KUISOMA KWA MARA YA KWANZA KWENYE UKURASA WA FESIBUKU WA KONA YA RIWAYA RELOADED "anastahiki pongezi kubwa kwa umahiri alio uonesha katika utunzi wake. Ameitendea haki tasnia hii ya uandishi wa riwaya." "ma ni noma, umenirudisha nchi ya kusadikikaaa a.k.a. kufikirika! HONGERA, hadithi ni nzuri.” “Mtunzi hii hadithi tulikuwa tukiisoma na shangazi zangu hapa nyumbani ama hakika wameipenda mno! Wewe ni kiboko.” “Ahsante mwandshi kwa riwaya nzuri na yenye kusisimua, ombi la kitabu tafadhali tujulishane kikiwa tayari.” “Umenikumbusha simulizi ya "binti chura' RTD wakati huo, hii ni simulizi ya kipekee kabisa...” “Duh...mtunzi wa Hii Kitu ni mtu mzito saaana, na anastahili pongezi kwa kweli!” “Ahsante sana mtunzi. Umetufanya tufurahi, lakini zaidi tumejifunza mengi sana. Tunawashukuru sana viongozi wa KONA YA RIWAYA RELOADED kwa kutuletea stori hii.” “Madhara, mapenzi, mateso, mauaji, unafki, ujasiri, uchawi, uongo, na vinginevyo vingi vinapatikana hapa kumaanisha fasihi imekamilika kwa mrembo wetu Sango, lkn nauliza itaendelea kitabuni? Ama ndio mwisho? Kwa sababu naona haijaisha mpaka Kibwe na Hanga wamalize kazi...” “Yaani kwa jinsi ilivyonivutia nimekuwa nikirudiarudia kuisoma mara mbili mbili. Safi sana mtunzi.” “Harakisha kitabu mama!” “Katika miaka yote ya KONA YA RIWAYA RELOADED, nadhani hii ndio simulizi inayoshika namba 1. Nadhani kama ni picha basi trela ndio linaanza! SANGO KIPOZI...unatisha mama!”

Sample Read

2,000 Tsh.

Bei

ALIKUWA ni mwanamke mzuri sana. Mwanamke mrefu, urefu usiochukiza. Alikuwa na sura ya duara. Nywele zake alikuwa amezikata vizuri ndogondogo, mtindo maarufu kama ungaunga. Alikuwa na umbo zuri lililotenganishwa na kiuno chembamba. Kifuani, alibeba maziwa madogo ya duara. Tumbo dogo, yale wayabebayo walimbwende. Chini, alikuwa na mapaja ya haja. Mapaja manene yanayojaa vyema katika suruali. Alikuwa na miguu minene. Miguu iitwayo ya bia. Alikuwa anatembea kwa mwendo wa madaha. Huku akiacha mwili wake ukitikisika vizuri sana kwa nyuma. Hizo ni sifa chache sana za mwanamke niliyekuwa namsubiri. Sikuwa na miadi nae. Nilikuwa namsubiri apite tu ili nimuone. Hakuwa mpenzi wangu. Sikuwa namjua kwa jina. Sikuwa najua anapokaa, lakini sikwenda kazini ili nimuone mwanamke ambaye nilitokea kumhusudu sana. Mwanamke aliyetokea kuuteka moyo wangu ghafla, kuzimeza fikra zangu. Cha ajabu, sasa saa saba hakuwa amepita. Alikuwa na kawaida ya kupita kila siku, saa tatu asubuhi, leo hii mpaka saa saba mchana alikuwa bado hajatokea. "Amepatwa na nini? Mbona mpaka sasahivi hajapita? Au anaumwa? Au amesafiri? Au leo amepita asubuhi sana.. Siku yoyote atakayopita lazima nimueleze jinsi ninavyoumia juu yake. Nimueleze nia yangu ya dhati ya kutaka kuwa nae. Awe wangu. Nimueleze kama ninampenda kuliko mwanamke yeyote yule hapa duniani. Nimueleze kuwa nataka kuishi na yeye milele. Nataka kuwa sehemu ya maisha yake, awe sehemu ya maisha yangu. Nataka anikaribishe katika moyo wake, niweke kambi. Tena kambi ya kudumu..." Nikiwa katikati ya mawazo ndipo nilipomuona akija. Moyo uliniripuka kwa furaha. Alikuwa amependeza kuliko siku zote. Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya Pinki. Blauzi nzuri yenye mistari meupe na meusi, rangi iliyofanana na mnyama Pundamilia. Mkononi alikuwa amebeba kibegi kidogo cheupe. Alikuwa anatembea kwa madaha kuja pale nilipokuwa nimekaa. Nilinyanyuka kitini huku nikisema

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

Miongoni mwa matukio makubwa yaliyofanyika katika Vita Vya Pili VyaDunia ni pamoja na ule uvamizi wa Majeshi ya Ushirika uliobatizwa jina la ‘Operesheni Kipondo (Operation Husky)’ dhidi ya kisiwa cha Sicily kilichopo nchini Italy. Shambulizi katika kisiwa hicho zilianza kwa kutumia idadi kubwa ya manowari na ndege za kivita kwa lengo la kuyarahisishia kazi majeshi ya ardhini yaliyoingia kisiwani humo baadaye na kukamilisha zoezi hilo kwa mafanikio makubwa huku idadi kubwa ya uongozi wa juu pamoja na wanajeshi wengi wa adui ikijumuisha majeshi ya kijerumani wakibahatika kukimbilia katika miji ya bara ya Taifa hilo lililokuwa likiongozwa na fashisti Benito Mussollin (Uvamizi huo ulianzia usiku wa tarehe 9/7/1943 hadi 10/7/1943 lakini vita vilimalizika rasmi tarehe 17/7/1943). Ushindi huo wa Majeshi ya Ushirika ulifungua ‘Mlango Wenye Usalama Wa Bahari Ya Mediterranean’ huku ukiwa umemdhoho sha sana Mussolini kiasi katika siku za mwishoni za mwezi huo wa Julai serikali yake ilipinduliwa; hatahivyo, mpango mwingine uliolenga kuvamia eneo lote la bara la Taifa hilo uliopewa jina la ‘Operesheni Banguko (Operation Avalanche)’ uliendelea kufanyiwa kazi.

Sample Read

0 Tsh.

Bei

Jinsi ya kutumia UWARIDI app

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Kidokezo Ni maisha yaliyojaa utata na mashaka makubwa. Maisha yaliyoandamwa na vita na majungu. Yote haya ni kwa sababu ya bidii aliyokuwa nayo kijana Ramson! Kijana huyu aliishi katika kijiji kiitwacho Taabu yanini. Asilimia kubwa ya wakazi wa kijiji hiki walikuwa ni wavivu. Uvivu wao ulipelekea kuona wivu kwa mafanikio ya kijana Ramson. Siku moja wanakijiji waliandamana kwenda nyumbani kwa Mzee Kihedu babu yake Ramson! Mwenyekiti na watu wake walimfukuza Ramson kwa kisingizio kuwa alikuwa ni mwizi! Kwa namna ya taabu alianza maisha Mbali na kijiji hiki kando ya bahari ya hindi. Mahali hapa alipata ubunifu wa kuutengeneza ufukwe huo kusudi ufae kutembelewa na watu kwa ajili ya mapumziko. Bidii yake ilimfanya afanikiwe na kupata watu wengi waliotembelea mahali hapo. Siku moja mtu mmoja tajiri alikuja na mkewe ufukweni hapo. Jina lake aliitwa Dr. Jackson Kigoi. Mke wake aliitwa Mary! Watu hawa walitokea kuupenda ufukwe huu. Baada ya muda Dr. Jackson alisafiri kwenda Uingereza kwa ajili ya kuongeza Elimu yake ya Udaktari. Hapo ndipo Mary mkewe alipoanza ushawishi wa kimapenzi kwa kijana huyu Ramson. Kwa shingo upande Kijana huyu aliingia kwenye uhusiano huo hali iliyosababisha kupatikana kwa mtoto.

Sample Read

4,000 Tsh.

Bei

Ni saa 12 asubuhi, jua linaanza kuchomoza binadamu, wanyama ndege na kila kiumbe vinaoneakana kuwa na uhai, baada ya mapumziko ya usingizi, kila mmoja anaonekana akianza shughuli zake ambazo amekusudia. Katika hali ya uchangamfu inayoonekana kupendeza zaidi kwa ndege wanaotoka katika viota vyao na kuanza kuimba na kuruka angani, pia wanyama wanaotoka vichakani na mafichoni mwao na kuanza mawindo ya kutafuta riziki zao. Hali kadhalika katika hali hii, asubuhi kunapokucha kila binadamu huwa anaamka na lake, wapo wanaoamka kwenda kusali, wapo wanaokwenda hospitali kutazama wagonjwa au kutibiwa, wanaokwenda baharini kuvua, maofisini na viwandani kufanya kazi, masokoni kuuza na kununua, mashambani kulima na kuvuna na wapo wanaokwenda vituo vya basi kwa ajili ya kusafiri. Kusafiri kwa sababu mbalimbali. Hali hii ya vurumai huonekana zaidi katika vituo vya usafiri wa mabasi, hasa vilivyopo mijini, Morogoro ikiwa mojawapo. Katika wasafiri ambao wamerauka alfajiri hiyo ya saa 12, wakawa wamekwishafika kituo cha basi cha Morogoro tayari kwa kusafiri, mmojawapo alikuwa ni Lilian Seuya.

Sample Read

7,000 Tsh.

Bei

Hali ya hewa haikuwa shwari katika jiji la Entebbe nchini Uganda, nyakati hizo za saa saba usiku kulikuwa na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha. Karaha hiyo iliongezeka katika mitaa ya matajiri wa jiji hilo kwani katika nyumba moja kulikuwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka. Kulikuwa na harakati za watu tofauti ambazo hazikuwa na mafanikio dhidi ya moto huo ulioshika nyumba hiyo huku ikiaminika kuwa ulisababishwa na hitilafu ya umeme. Watu waliokuwapo nje ya nyumba hiyo walikuwa wakihofia uhai wao kujitosa katika moto huo kuokoa maisha ya wanafamilia hao waliokuwa wakipiga kelele za kuomba msaada.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

N aitwa Tigga Mumba. Marafiki zangu walizoea kuniita “Tigga-Mu”. Lakini sasa sina marafiki tena. Mimi ni mtafiti wa mambo ya kale...lakini nadhani niseme kuwa nilikuwa mtafiti wa mambo ya kale...Archaelogist. Nilikuwa nina matarajio makubwa sana maishani. Nikiwa na shahada yangu ya kwanza ya utafiti wa mambo ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kazi nzuri na ninayoipenda, marafiki wachache lakini wazuri na wacheshi, jamii yangu ndogo iliyojaa upendo, na mchumba mtanashati niliyekuwa natarajia kufunga naye ndoa itakayojaa upendo, nikiwa na ndoto ya kuzaa naye watoto wawili: wa kwanza wa kike na wa pili wa kiume...sikuwa na sababu ya kukosa matarajio makubwa maishani. Lakini vyote hivi vilikuja kutoweka ghafla katika tukio moja tu la kutisha na kuogopesha sana lililotokea katikati ya msitu mnene ulioko katikati ya nchi hii...siku moja nilikuwa msichana mmoja mcheshi wa miaka ishirini na saba, mwenye urembo wa kuridhisha na ndoto nyingi za mafanikio mbele yangu, siku iliyofuata vyote hivi viligeuka na kuwa ndoto moja mbaya na ya kutisha sana. Ila tu mambo yaliyobadilisha matarajio na maisha yangu hayakuwa ndoto bali ni kweli kabisa. Ni vigumu sana kuamini kuwa mambo yaliyonitokea...na yanayoendelea kunitokea, yananitokea mimi. Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na kuniwia vigumu kuamini kuwa ninatokewa na mambo haya, bado najikuta kuwa ni mimi peke yangu ndiye ninayeamini ukweli wa matukio haya ya kutisha. Kwani kila ninapokwenda, kila ninapojaribu kuelezea ukweli wa matukio haya, hakuna hata mmoja anayeniamini...na naishia kuwa mkimbizi ninayekimbia kwa woga na wasiwasi. Na kama hiyo haitoshi, kinachouma kuliko vyote ni kwamba kwa mtu niliyekuwa na marafiki, jamaa na hata mchumba wa dhati, najikuta nikilazimika kukabiliana na masahibu haya peke yangu. Yote hii ni kwa sababu ya kushuhudia tukio moja la kutisha lililotokea katikati ya msitu mnene. Tukio lililonifanya niwe mkimbizi ndani ya nchi yangu...kwa sababu sasa sina mahala popote ambapo ninaweza kujihisi salama, sina mtu yeyote ambaye nitajihisi salama kuwa naye, na wala hakuna mazingira yoyote yanayoweza kunifanya nijione salama. Mahala pekee ambapo nitajihisi salama ni pale nitakapokuwa peke yangu...na mtu pekee nitakayejihisi salama kuwa naye ni mimi mwenyewe! Na mpaka nitakapoipata hiyo sehemu ya peke yangu, nitabaki kuwa mkimbizi tu...peke yangu, muoga, mpweke! Na hata hapa ninapoandika maelezo haya kuhusu tukio la kutisha lililobadili kabisa mwelekeo wa maisha yangu na mtazamo wangu katika maisha kwa ujumla, niko peke yangu. Nikiwa na mtu pekee ninayemuamini katika maisha yangu...Tigga Mumba. Peke yangu... Niliyejawa woga...Nisiye na kwangu... Mkimbizi...

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Kwa wapendanao. Ni vigumu kuueleza upendo wa kweli kwa maneno, ila matendo huudhihirisha kwa namna ya kipekee sana. upendo ni kitu kisichoonekana kwa macho ila hisia hukipelekea kuonekana kupitia matendo ya wapendanao. Siri ya kitu hiki kiitwacho upendo nani aijuaye kwa yakini? Nani ajuaye kuwa apaswa kumpenda nani katika upendo halisi unaozaa ndoa? Upendo sio kutamani, wala hauna sura hiyo. Upendo wa kweli huona kengeza badala ya chongo kwa yule aliyeangukiwa na kitu hicho cha thamani. Upendo wa kweli huonekana wakati mmoja anapopata matatizo. Upendo wakati wa raha na utele wa mali kamwe sio halisi. Dunia yetu kwa wakati huu umejaa durufu nyingi za upendo, upendo wa mitandaoni, upendo wa uongo na mapambo ya kitapeli. Dunia tuliyo nayo inahitaji upendo wa kweli uliobeba thamani halisi. Thamani isiyonunulika kwa fedha wala dhahabu. Upendo ambao mwandishi wa kitabu hiki ameamua kuuita “Upendo kutoka sayari nyingine!!” Upendo kama huu wanadamu wanauhitaji kama vile maji katika jagwa!

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Wakati wa majira ya saa sita mchana, hali ya hewa ilikuwa shwari katika jiji la Dar es salaam lililotawaliwa na jua kiasi. Watu walionekana wakiwa katika mihangaiko yao ya kujitafutia riziki katika kipindi hicho cha mwezi wa kumi na mbili. Akili zao zilikuwa zimetawaliwa na mawazo juu ya sikukuu za mwisho wa mwaka ambazo walipaswa kuzigharamia ili kwenda sawa na utamaduni wa kila mwaka. Lamos Maputo, akiwa kijana miaka thelathini na saba alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa katika pilikapilika za mihangaiko hiyo ya mwisho wa mwaka. Akiwa mwenyeji wa Shinyanga, tayari alikuwapo jijini na familia yake kwa miezi kadhaa akijitafutia riziki. Ugumu wa maisha kwa kipindi cha miaka mingi ndio uliomchanganya Lamos kwani hata wakati huo alionekana akiongea peke yake. Alikuwa amebeba kikapu kikubwa ambacho kilikuwa na samaki ndani yake aliowanunua eneo la Feri, Posta. Huku akiwa katika mavazi duni, kikapu hicho kilionekana kikichuruzika maji ambayo yalikuwa yakiendelea kulowanisha shati lake alilokuwa amevaa. Kodi ya nyumba, afya ya mwanae pamoja na biashara yake iliyokuwa inasuasua ndivyo vitu vilivyosababisha awe anaongea peke yake barabarani. Wakati huo alikuwa amepewa siku tatu tu ili akamilishe kodi ya nyumba aliyokuwa amepanga Kimara, huku akielezwa kuwa angefukuzwa kama angeshindwa kutimiza agizo hilo. Mwanaye pekee Veronika alikuwa na matatizo ya kiafya kwani naye alikuwa uvimbe mkubwa kichwani mwake. Mtoto huyo aliyekuwa na mwaka mmoja alimchanganya zaidi Lamos kwani uvimbe wake ulikuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Sample Read