5,000 Tsh.

Bei

Wakati wa majira ya saa sita mchana, hali ya hewa ilikuwa shwari katika jiji la Dar es salaam lililotawaliwa na jua kiasi. Watu walionekana wakiwa katika mihangaiko yao ya kujitafutia riziki katika kipindi hicho cha mwezi wa kumi na mbili. Akili zao zilikuwa zimetawaliwa na mawazo juu ya sikukuu za mwisho wa mwaka ambazo walipaswa kuzigharamia ili kwenda sawa na utamaduni wa kila mwaka. Lamos Maputo, akiwa kijana miaka thelathini na saba alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa katika pilikapilika za mihangaiko hiyo ya mwisho wa mwaka. Akiwa mwenyeji wa Shinyanga, tayari alikuwapo jijini na familia yake kwa miezi kadhaa akijitafutia riziki. Ugumu wa maisha kwa kipindi cha miaka mingi ndio uliomchanganya Lamos kwani hata wakati huo alionekana akiongea peke yake. Alikuwa amebeba kikapu kikubwa ambacho kilikuwa na samaki ndani yake aliowanunua eneo la Feri, Posta. Huku akiwa katika mavazi duni, kikapu hicho kilionekana kikichuruzika maji ambayo yalikuwa yakiendelea kulowanisha shati lake alilokuwa amevaa. Kodi ya nyumba, afya ya mwanae pamoja na biashara yake iliyokuwa inasuasua ndivyo vitu vilivyosababisha awe anaongea peke yake barabarani. Wakati huo alikuwa amepewa siku tatu tu ili akamilishe kodi ya nyumba aliyokuwa amepanga Kimara, huku akielezwa kuwa angefukuzwa kama angeshindwa kutimiza agizo hilo. Mwanaye pekee Veronika alikuwa na matatizo ya kiafya kwani naye alikuwa uvimbe mkubwa kichwani mwake. Mtoto huyo aliyekuwa na mwaka mmoja alimchanganya zaidi Lamos kwani uvimbe wake ulikuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI RAYMOND MWALONGO

7,000 Tsh.

Bei

Hali ya hewa haikuwa shwari katika jiji la Entebbe nchini Uganda, nyakati hizo za saa saba usiku kulikuwa na mvua kubwa ya mawe iliyonyesha. Karaha hiyo iliongezeka katika mitaa ya matajiri wa jiji hilo kwani katika nyumba moja kulikuwa na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka. Kulikuwa na harakati za watu tofauti ambazo hazikuwa na mafanikio dhidi ya moto huo ulioshika nyumba hiyo huku ikiaminika kuwa ulisababishwa na hitilafu ya umeme. Watu waliokuwapo nje ya nyumba hiyo walikuwa wakihofia uhai wao kujitosa katika moto huo kuokoa maisha ya wanafamilia hao waliokuwa wakipiga kelele za kuomba msaada.

Sample Read