6,000 Tsh.

Bei

N aitwa Tigga Mumba. Marafiki zangu walizoea kuniita Tigga-Mu. Lakini sasa sina marafiki tena. Mimi ni mtafiti wa mambo ya kale...lakini nadhani niseme kuwa nilikuwa mtafiti wa mambo ya kale...Archaelogist. Nilikuwa nina matarajio makubwa sana maishani. Nikiwa na shahada yangu ya kwanza ya utafiti wa mambo ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kazi nzuri na ninayoipenda, marafiki wachache lakini wazuri na wacheshi, jamii yangu ndogo iliyojaa upendo, na mchumba mtanashati niliyekuwa natarajia kufunga naye ndoa itakayojaa upendo, nikiwa na ndoto ya kuzaa naye watoto wawili: wa kwanza wa kike na wa pili wa kiume...sikuwa na sababu ya kukosa matarajio makubwa maishani. Lakini vyote hivi vilikuja kutoweka ghafla katika tukio moja tu la kutisha na kuogopesha sana lililotokea katikati ya msitu mnene ulioko katikati ya nchi hii...siku moja nilikuwa msichana mmoja mcheshi wa miaka ishirini na saba, mwenye urembo wa kuridhisha na ndoto nyingi za mafanikio mbele yangu, siku iliyofuata vyote hivi viligeuka na kuwa ndoto moja mbaya na ya kutisha sana. Ila tu mambo yaliyobadilisha matarajio na maisha yangu hayakuwa ndoto bali ni kweli kabisa. Ni vigumu sana kuamini kuwa mambo yaliyonitokea...na yanayoendelea kunitokea, yananitokea mimi. Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na kuniwia vigumu kuamini kuwa ninatokewa na mambo haya, bado najikuta kuwa ni mimi peke yangu ndiye ninayeamini ukweli wa matukio haya ya kutisha. Kwani kila ninapokwenda, kila ninapojaribu kuelezea ukweli wa matukio haya, hakuna hata mmoja anayeniamini...na naishia kuwa mkimbizi ninayekimbia kwa woga na wasiwasi. Na kama hiyo haitoshi, kinachouma kuliko vyote ni kwamba kwa mtu niliyekuwa na marafiki, jamaa na hata mchumba wa dhati, najikuta nikilazimika kukabiliana na masahibu haya peke yangu. Yote hii ni kwa sababu ya kushuhudia tukio moja la kutisha lililotokea katikati ya msitu mnene. Tukio lililonifanya niwe mkimbizi ndani ya nchi yangu...kwa sababu sasa sina mahala popote ambapo ninaweza kujihisi salama, sina mtu yeyote ambaye nitajihisi salama kuwa naye, na wala hakuna mazingira yoyote yanayoweza kunifanya nijione salama. Mahala pekee ambapo nitajihisi salama ni pale nitakapokuwa peke yangu...na mtu pekee nitakayejihisi salama kuwa naye ni mimi mwenyewe! Na mpaka nitakapoipata hiyo sehemu ya peke yangu, nitabaki kuwa mkimbizi tu...peke yangu, muoga, mpweke! Na hata hapa ninapoandika maelezo haya kuhusu tukio la kutisha lililobadili kabisa mwelekeo wa maisha yangu na mtazamo wangu katika maisha kwa ujumla, niko peke yangu. Nikiwa na mtu pekee ninayemuamini katika maisha yangu...Tigga Mumba. Peke yangu... Niliyejawa woga...Nisiye na kwangu... Mkimbizi...

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI HUSSEIN TUWA

7,000 Tsh.

Bei

“Tuwa unataka niseme nini zaidi ya saluti?” “Ama kweli Hussein Tuwa unatukonga vilivyo,tunashukuru sana.” “Safi kaka! MTAFITI inatuliwaza sana. Pia inatusisimua.” “Dah! Hii riwaya kiukweli ni KUNTUU!” “I salute you, mkubwa. Hakika unaweza.” “Hii hadithi inaendelea kuwa nzuri kila siku! Kuikosa ni hatariiii!!!” “Jaman hadith hii kama isiishe vile, lakini ndo haiwezekani.Kaka unatisha. Nimeupenda sana mtiririko wa matukio BIG UP!” “Hakika kaka HUSENI TUWA riwaya zako ni nzuri sana natamani sana kukikamata kitabu cha hii riwaya ili nifaidi uhondo huu mwanzo mwisho.” “Duh, hii ni zaidi ya bongo movie kwa sababu hauwezi kutabiri next panatokea nini. Hongera sana Bradha.” “Bonge la movie! Ninaposoma utafikiri nipo ndani ya New world Cinema naangalia Movie...Thumbs Up, Bwana Tuwa.” “Unpredictable novel! BIG UP to the Author.” “Tuwa upo juu! Hii kazi imejaa ufundi wa hali ya juu sana. M/ mungu akuzidishie kaka!” “Haaa! Hussein Tuwa yaani wanimaliza ujue? You make me feel nipo Afrika kabisaaa! Yaani nakuvulia kofia.” “Nashukuru kwa kuipata kona ya riwaya reloaded kwani nilipoteza matumaini ya kuendelea na riwaya hii ya kusisimua na yenye mandhari halisi ya maisha yetu watanzania. Hongera sana mtunzi.” “Unanikumbusha sana enzi zile tukikusubiri uje kulala home kutoka Chuo, tupate mi-movie ya kusisimua.You were born to tell stories my brother!”-Kareem Tuwa “Kaka Tuwa unatambaa futi 70000 toka usawa wa bahari. Hii MTAFITI ni balaa tupu aisee. Thumbs Up, HT.” “Hili ni bonge moja la stori kaka. Kama vipi tuletee na kitabu chake kabisa, tupate kwenda sawa.” MTAFITI

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

UKUNGU MZITO UMEMTANDA kwenye jicho lake la kushoto. Anahisi jinsi lilivyovimba kutokana na uzito wa jicho lile pale usoni kwake akilinganisha na jicho lakejingine. Haoni vizuri. Mvumo mkali, unavuma masikioni mwake na kuzifanya kelele za watazamaji waliofurika ukumbini zisikike kana kwamba zinatokea ndani maji ya bwawa lililofurika... au kana kwamba yeye anazisikia kelele zile akiwa amezamishwa chini kabisa ya bwawa lenye kina kirefu. Hasikii vizuri. Kichwa kinamgonga. Sana, mfululizo. Kinamuwia uzito kuliko alivyopata kuhisi maishani mwake. Anakitikisa kwa nguvu na kututumua jicho lake moja linalofanya kazi kwa wakati ule ili aweze kuona vizuri. Anamuona mpinzani wake akitumia kamba za ulingo kujiinua kwa taabu kutoka kwenye sakafu ya ulingo ule waliokuwamo. Anainuka! Haamini hali ile. Hata baada ya kumtwanga ile ngumi ambayo huwa haimuachii mtu uwezo wa kuinuka tena? Kweli? Kweli. Mpinzani wake anafanikiwa kuinuka na kumgeukia akiwa ameinua mikono tayari kuendelea na pambano. Mwamuzi anamuwahi na kumzuia. Anamuuliza kitu huku akimuoneshea vidole viwili mbele ya uso wake. Mpinzani anatoa jibu. Mwamuzi anaonekana kuridhishwa na jibu lake. Yaani hata baada ya kichapo chote kile kilichoishia kwenye ile ngumi aliyoamini kuwa ndio ingemaliza pambano bado jamaa kaweza kuona vile ni vidole vingapi! Mambo mawili yanamfunukia kwa wakati mmoja akilini mwake. Kwanza anaona jinsi uso wa mpinzani wake ulivyochakaa kwa kipigo alichomshushia. Ulikuwa umetutumka kwa manundu. Macho yake yote mawili yalikuwa yamemvimba vibaya ilhali mdomo wake wa juu ukiwa umeumuka vilivyo, na kinywa chake kikiwa kimelowa damu. Pili anahisi ile sakafu iliyowambwa ya ule ulingo waliokuwamo ikiingia mabonde, naye anashindwa kusimama vizuri juu yake. Anayumba. Anamuona... kwa shida... mwamuzi akiziweka ngumi za mpinzani wake

Sample Read

7,000 Tsh.

Bei

Ni miaka mitatu tangu kuuawa kwa Osama bin Laden nchini Pakistani. Wanamgambo wa Al-Qaida walikuwa wamesambaratika. Wengi miongoni mwao wakiwa wameuawa, ilhali wengine wakikamatwa na majeshi ya Marekani nchini Pakistani... na kikundi cha wachache wengine kikiwa kimefanikiwa kutoroka na kukimbilia eneo la Waziristani lililo kaskazini mwa Pakistani, kwenye kitongoji cha Miramshah kilichokuwa kinadhibitiwa na washirika wao wakuu, wapiganaji wa Taleban. Huko wakapata hifadhi baada ya kifo kile kichungu cha kiongozi wao. Na tangu wakati huo, hali ya wakaazi wa kijiji kilichokuwa kiasi cha kilomita saba kutoka kwenye ile ngome ya watalebani iliyowahifadhi wale wanamgambo wachache wa Al-Qaida, imekuwa ni ya mashaka makubwa. Njaa ilikuwa imetawala, mahitaji yote muhimu yakatoweka, maradhi hayakuwa na wa kuyatibu, magonjwa ya mlipuko na yatokanayo na lishe duni yakishamiri...

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

MESEJI ZA SIMU KUHUSU MDUNGUAJI KUTOKA KWA BAADHI YA WASOMAJI WAKATI RIWAYA HII ILIPOTAKA KWA MARA YA KWANZA KWENYE GAZETI LA KIU YA JIBU MWAKA 2006: Duuh! Hii ni baab kubwa mzee mwenyewe. Hadi tunaunguza mboga kwa kusoma Mdunguaji! Endelea kutupa uhondo huu adimu nchini.Big Up Tuwa. Big Up sana mtu wangu, THE SNIPER ni mfuniko mnene. Imebana vilivyo na nategemea uhondo zaidi. Tremendous pressure, even to the very best! Wape akina Sword sh, Honey B na Stealth relief kidogo Mr. Tuwa! Mambo vipi bro? Mzee unatisha MDUNGUAJI imenishika vibaya sana! Big Up! Keep it Up! Hi! Babu kama vipi tuandalie kitabu, THE SNIPER ni noma mzee. Tumekukubali. Tuwa nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa riwaya zako lakini MDUNGUAJI imevunja rekodi. Kweli una kiri sana na una uwezo mkubwa wa kujenga visa sisimuzi. Mambo yako yatakuwa sa . Sisi wapenzi wa riwaya zako tunaomba THE SNIPER uitolee kitabu. Ebwana mtu wangu unazidi kunidatisha na riwaya yako ya THE SNIPER. Mwana mi bado nipo nawe, vipi kitabu lini? Baba naikubali hii riwaya yako (Mdunguaji).Maoni yangu kabla haijakwisha tupate kitabu. Bw. Tuwa nadhani ukitoa tuzo kwa wasomaji bora, na imani nami nitakuwa mmoja wao, hivyo ushauri wangu na THE SNIPER iweke kwenye kitabu tupate uhondo kwa pamoja, au tunga vitabu tu mbona tushakukubali na tunajua kuwa we ndio bingwa kwa riwaya zinazosisimua nchini? Ebwana mambo vipi mzee Tuwa? Mwanzo ulikuwa unanichanganya lakini sasa unanipa ile kitu roho inapenda. (THE SNIPER) inatisha. Kaza buti mzazi,tuko pamoja. Hussein Tuwa sina ushauri wala maoni isipokuwa kukupongeza kwa kipaji chako. Hongera sana man. Mimi ni mwanajeshi. Namfagilia sana Baddi Gobbos, natamani kuwa kama yeye.

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Riwaya hii imejumuisha sehemu zote mbili za kisa hiki, yaani PART 1 na PART 2 kwa pamoja, kinyume na namna kilivyotoka kwenye kitabu kigumu ambapo vilitoka vitabu viwili tofauti kila kimoja kikiuzwa elfu 8. Sasa hapa unapata kisa cha vitabu vyote viwili kwa elfu 8 tu

Sample Read