4,000 Tsh.

Bei

Ni saa 12 asubuhi, jua linaanza kuchomoza binadamu, wanyama ndege na kila kiumbe vinaoneakana kuwa na uhai, baada ya mapumziko ya usingizi, kila mmoja anaonekana akianza shughuli zake ambazo amekusudia. Katika hali ya uchangamfu inayoonekana kupendeza zaidi kwa ndege wanaotoka katika viota vyao na kuanza kuimba na kuruka angani, pia wanyama wanaotoka vichakani na mafichoni mwao na kuanza mawindo ya kutafuta riziki zao. Hali kadhalika katika hali hii, asubuhi kunapokucha kila binadamu huwa anaamka na lake, wapo wanaoamka kwenda kusali, wapo wanaokwenda hospitali kutazama wagonjwa au kutibiwa, wanaokwenda baharini kuvua, maofisini na viwandani kufanya kazi, masokoni kuuza na kununua, mashambani kulima na kuvuna na wapo wanaokwenda vituo vya basi kwa ajili ya kusafiri. Kusafiri kwa sababu mbalimbali. Hali hii ya vurumai huonekana zaidi katika vituo vya usafiri wa mabasi, hasa vilivyopo mijini, Morogoro ikiwa mojawapo. Katika wasafiri ambao wamerauka alfajiri hiyo ya saa 12, wakawa wamekwishafika kituo cha basi cha Morogoro tayari kwa kusafiri, mmojawapo alikuwa ni Lilian Seuya.

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI AMRI BAWJI