6,000 Tsh.

Bei

Kidokezo Ni maisha yaliyojaa utata na mashaka makubwa. Maisha yaliyoandamwa na vita na majungu. Yote haya ni kwa sababu ya bidii aliyokuwa nayo kijana Ramson! Kijana huyu aliishi katika kijiji kiitwacho Taabu yanini. Asilimia kubwa ya wakazi wa kijiji hiki walikuwa ni wavivu. Uvivu wao ulipelekea kuona wivu kwa mafanikio ya kijana Ramson. Siku moja wanakijiji waliandamana kwenda nyumbani kwa Mzee Kihedu babu yake Ramson! Mwenyekiti na watu wake walimfukuza Ramson kwa kisingizio kuwa alikuwa ni mwizi! Kwa namna ya taabu alianza maisha Mbali na kijiji hiki kando ya bahari ya hindi. Mahali hapa alipata ubunifu wa kuutengeneza ufukwe huo kusudi ufae kutembelewa na watu kwa ajili ya mapumziko. Bidii yake ilimfanya afanikiwe na kupata watu wengi waliotembelea mahali hapo. Siku moja mtu mmoja tajiri alikuja na mkewe ufukweni hapo. Jina lake aliitwa Dr. Jackson Kigoi. Mke wake aliitwa Mary! Watu hawa walitokea kuupenda ufukwe huu. Baada ya muda Dr. Jackson alisafiri kwenda Uingereza kwa ajili ya kuongeza Elimu yake ya Udaktari. Hapo ndipo Mary mkewe alipoanza ushawishi wa kimapenzi kwa kijana huyu Ramson. Kwa shingo upande Kijana huyu aliingia kwenye uhusiano huo hali iliyosababisha kupatikana kwa mtoto.

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI ANDREW MHINA

4,000 Tsh.

Bei

Wakati dunia ikihaha kutokana na upungufu wa ajira duniani, hali inabadilika ghafla na kuwafanya wasomi kukosa jibu kwa elimu zao. Hapa ndipo vyeti vinavyodhibitisha elimu za wasomi hawa toka kila kona ya dunia kuwa ni bure kabisa. Ugunduzi wa vifaa maalumu vya kurahisisha kazi maofisini, vikiwepo computer na maroboti ya kila aina ndio sababu ya kukwama kwa ajira nyingi. Sio jambo la kificho tena kuwa wasomi kutoka vyuo vikuu na vile vya kati wapo kwenye changamoto ya aina yake. Lakini kwa upande mwingine Ujasiriamali umekuwa ndilo jibu pekee na suluhisho la uchumi duniani. Dunia sasa inapokea watu wenye nguvu ya vipaji kuwa sehemu ya uponyaji wa uchumi. Kwa hakika Ujasiriamali ndilo jibu hasa kwa dunia ya leo. Ndani ya kitabu hiki kuna mengi yaliyoainishwa ili kutoa njia ya namna ya kuuponya uchumi wako. Fursa ziko nyingi za kukufanya uhesabiwe kuwa bilioni baada ya miaka michache. Mafanikio ya nayopatikana kwenye ujasiriamali ni tofauti sana na yale yanayopatikana kwenye ajira ya mwajiriwa. Utajiri wa mjasiriamali hauna maswali wala hisia za kifisadi! Hili ndilo jibu pekee sana kwa kila mtubila kujalisha amesoma ama la. Kwa mengi ya thamani kubwa karibu ndani ya kurasa za kitabu hiki cha aina yake.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Kwa wapendanao. Ni vigumu kuueleza upendo wa kweli kwa maneno, ila matendo huudhihirisha kwa namna ya kipekee sana. upendo ni kitu kisichoonekana kwa macho ila hisia hukipelekea kuonekana kupitia matendo ya wapendanao. Siri ya kitu hiki kiitwacho upendo nani aijuaye kwa yakini? Nani ajuaye kuwa apaswa kumpenda nani katika upendo halisi unaozaa ndoa? Upendo sio kutamani, wala hauna sura hiyo. Upendo wa kweli huona kengeza badala ya chongo kwa yule aliyeangukiwa na kitu hicho cha thamani. Upendo wa kweli huonekana wakati mmoja anapopata matatizo. Upendo wakati wa raha na utele wa mali kamwe sio halisi. Dunia yetu kwa wakati huu umejaa durufu nyingi za upendo, upendo wa mitandaoni, upendo wa uongo na mapambo ya kitapeli. Dunia tuliyo nayo inahitaji upendo wa kweli uliobeba thamani halisi. Thamani isiyonunulika kwa fedha wala dhahabu. Upendo ambao mwandishi wa kitabu hiki ameamua kuuita “Upendo kutoka sayari nyingine!!” Upendo kama huu wanadamu wanauhitaji kama vile maji katika jagwa!

Sample Read