3,000 Tsh.

Bei

Chifu Abdullah anaingia katika kazi ngumu kuliko zote alizowahi kuzifanya katika maisha yake, kazi ya kuusaka mkanda wa siri uliopotea kimaajabu katika kasri yake. Alishindwa kuulinda, sasa anausaka kwa nguvu. Msako wa mkanda unazikutanisha pande mbili zenye taaluma za juu katika mambo ya uhalifu. Mkanda unatembea toka kwenye mkono huu kwenda katika mkono mwengine, pande zote mbili zinautafuta mkanda kwa nguvu na akili kila unapopita. Wengi wanajeruhiwa, wengi wanaumizwa, wengi wanakufa, sababu kuu ni Mkanda wa Siri. Jeshi la Polisi nalo linaingia kazini kusaka wahalifu, bila kujua wahalifu hao wana uhusiano mkubwa na Mkanda wa Siri. Haiwi kazi rahisi kuupata mkanda, mkanda unazua kizaazaa kwa maana sahihi ya neno kizaazaa. Hivi ndani ya mkanda wa siri kuna nini cha siri? Funua ndani upate majibu...

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI HALFANI SUDY

3,000 Tsh.

Bei

Ni asubuhi na mapema ndani ya mji wa Mafinga uliopo mkoani Iringa, Tanzania. Baridi likiwa kali sana. Watu walikuwa wanatembea mitaani huku wakiwa wamevaa makoti makubwa kupambana na baridi hiyo. Katika hoteli moja iliyopo katika mtaa wa Pipeline ndani ya mji huo kulikuwa na kikao cha siri cha watu wawili. Saa tatu sasa walikuwa wanapanga mikakati yao. "Sasa Martin fanya juu chini umpate Elizabeth Neville, ni yeye pekee ndio anajua kila kitu kuhusu mimi, na nina hakika endapo atathubutu tu kusema basi nimeangamia na ndoto yangu ya kuja kuwa rais wa Tanzania itakuwa imefikia kikomo." Lucas alisema kwa sauti ya upole na kusisitiza. "Usiwe na hofu yoyote Mheshimiwa Lucas. Mimi ndiye Martin, sijawahi kushindwa kazi yoyote ile. Ukiwa na tatizo lolote lile jua lifikapo kwa Martin limekwisha. Nipe siku tatu tu nitakuletea Elizabeth Neville mikononi mwako na utaamua mwenyewe nini cha kumfanya. Nakuhakikishia siri yako haitotoka katika mdomo wa Elizabeth Neville kwenda katika sikio lolote lile lingine hapa duniani." Martin alisema kwa kujiamini. "Nakuamini Martin Hisia. Sasa nakupa hizi milioni kumi za awali, na nitakupa milioni kumi na tano baada ya kukamilisha kazi hii. So milioni ishirini na tano ulizozihitaji zitakuwa zimekamilika" Lucas alisema huku akimkabidhi Martin bahasha yenye milioni kumi. Martin alizipokea, wakaagana. "Huyo Elizabeth Neville atakuwa anaijua siri gani ya waziri?. Maana kumpeleka kwake hiko kiumbe dhaifu tu katoa milioni ishirini na tano. Nitaifanya kazi hii siku mbili tu ili animalizie milioni zangu kumi na tano nilale mbele." Martin aliwaza akiwa ndani ya gari yake.

Sample Read

2,000 Tsh.

Bei

ALIKUWA ni mwanamke mzuri sana. Mwanamke mrefu, urefu usiochukiza. Alikuwa na sura ya duara. Nywele zake alikuwa amezikata vizuri ndogondogo, mtindo maarufu kama ungaunga. Alikuwa na umbo zuri lililotenganishwa na kiuno chembamba. Kifuani, alibeba maziwa madogo ya duara. Tumbo dogo, yale wayabebayo walimbwende. Chini, alikuwa na mapaja ya haja. Mapaja manene yanayojaa vyema katika suruali. Alikuwa na miguu minene. Miguu iitwayo ya bia. Alikuwa anatembea kwa mwendo wa madaha. Huku akiacha mwili wake ukitikisika vizuri sana kwa nyuma. Hizo ni sifa chache sana za mwanamke niliyekuwa namsubiri. Sikuwa na miadi nae. Nilikuwa namsubiri apite tu ili nimuone. Hakuwa mpenzi wangu. Sikuwa namjua kwa jina. Sikuwa najua anapokaa, lakini sikwenda kazini ili nimuone mwanamke ambaye nilitokea kumhusudu sana. Mwanamke aliyetokea kuuteka moyo wangu ghafla, kuzimeza fikra zangu. Cha ajabu, sasa saa saba hakuwa amepita. Alikuwa na kawaida ya kupita kila siku, saa tatu asubuhi, leo hii mpaka saa saba mchana alikuwa bado hajatokea. "Amepatwa na nini? Mbona mpaka sasahivi hajapita? Au anaumwa? Au amesafiri? Au leo amepita asubuhi sana.. Siku yoyote atakayopita lazima nimueleze jinsi ninavyoumia juu yake. Nimueleze nia yangu ya dhati ya kutaka kuwa nae. Awe wangu. Nimueleze kama ninampenda kuliko mwanamke yeyote yule hapa duniani. Nimueleze kuwa nataka kuishi na yeye milele. Nataka kuwa sehemu ya maisha yake, awe sehemu ya maisha yangu. Nataka anikaribishe katika moyo wake, niweke kambi. Tena kambi ya kudumu..." Nikiwa katikati ya mawazo ndipo nilipomuona akija. Moyo uliniripuka kwa furaha. Alikuwa amependeza kuliko siku zote. Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya Pinki. Blauzi nzuri yenye mistari meupe na meusi, rangi iliyofanana na mnyama Pundamilia. Mkononi alikuwa amebeba kibegi kidogo cheupe. Alikuwa anatembea kwa madaha kuja pale nilipokuwa nimekaa. Nilinyanyuka kitini huku nikisema

Sample Read