3,000 Tsh.

Bei

Hatua za maisha ya msichana hufanana sana na maisha ya Kipepeo aishiye na kukua katikati ya wadudu au viumbe wenye hila. Adui mkubwa wa Kipepeo anajitokeza, huyu ni Kinyonga aliyejificha ndani ya maua mazuri. Je, Kipepeo ataweza kuzitimiza ndoto zake katikati ya VINYONGA wenye njaa na kiu ya kumtafuna? Mfululizo wa riwaya hii unayamulika maisha ya kila msichana aishiye katika uso wa Dunia. Sehemu hii ya kwanza ambayo ni HAMANIKO inayaangaza maisha ya msichana LOLA, binti wa Majaliwa mwenye ndoto za lukuki. Kwa hila anabakwa siku ya mkesha wa Noeli baada ya kutiliwa dawa za kulevya kwenye soda. Baadaye Lola anashika ujauzito kisha jamii inamkataa na kumtenga kwa upofu wa sheria za kijiji chake. Hamaniko linamjaa moyoni, hamjui baba wa ujauzito aliokuwa pia hofu ya ndoto zake kumpotea. Lola hafi moyo anapambana kuyaunga maisha yake yaliyo chakaa. Je, Lola atapata nafasi ya kuyaungaunga maisha yake yaliyochakaa kama cheni na kuzitimiza ndoto zake pasipo kikwazo? Usiache kufuatilia mfululizo wa kisa hiki cha kusisimua na kuelimisha.

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI JOHN WISSE

3,000 Tsh.

Bei

Vijana wawili wanapendana hatimaye kuzama kwenye msitu mnene wa mahaba. Miaka minane inakatika wakiwa kama ndizi kwenye mkungu wake wakipeana kwa hamu. Siku inatokea msichana anawaza hatma ya mapenzi yao pasipo ndoa, anaamua kumuuliza mpenziwe juu ya kutaka kumfanya mkewe………anajibiwa kwa swali ambalo lilizaa jina la riwaya hii..”Kwa nini nikuoe wewe?” Baada ya swali hilo, mambo yanageuka na kuwa kindumbwendumbwe, kulikoni!!! ONJA KIDOGO MAZUNGUMZO YAO HAPA Kwa nini niliamua kumvulia nguo Rich wakati si mume wangu? Akiniacha je, itakuwaje? Hapana, ni vema nichukue hatua. Miaka minane ni mingi sana hasa ukizingatia wanaume maarufu kama huyu ni majanga matupu. Leo anaweza kuwa na mimi, kesho na mwingine na keshokutwa pia. Ananiwazia nini mtu huyu. Je ananipenda kama vile nampenda? Hapana, lazima niujue ukweli leo pasipo kificho.” Ha! Rose alijikuta akijawa na hamu ya kuuliza swali. Alitaka kujua hatma ya uhusino wao huo wenye furaha. Haya, Rose anauvunja ukimya hapa; Rose: Richard! Dear! (Alimtikisa) Rich: Hey! Vipi mpenzi! Rose: Amka bwana. Umelewa? Rich: Acha uzushi bwana. Nilewe nini tena? Nimepumzika tu mpenzi. Huoni leo ni faragha yetu kushinda zote? Huna budi kufanya hivyo, tulale. Rose: Kuna jambo nataka tulizungumze mpenzi. Nyanyuka basi nikueleze!(Wakati huo, Rose alimshika mkono Richard kumnyanyua na wote waliketi kitandani. Rose alimwegemea Richard kifuani huku mkono wake ukizichezea sharafa zake. Wakati hajaongea lolote, Rose alishikwa na kigugumizi). Rich alilianzisha; Rich: Mh! Nieleze basi dear, nini kinakusibu? Rose: Ah-m! Anyway, Rich- kuna jambo nataka kukueleza! Rich: Ok! Endelea! Rose: Nimezungukwa na furaha mwili wangu wote kwa ajili yako. Umeyafanya maisha yangu yawe na furaha hadi leo. Nina jambo naomba nikuulize mpenzi. Please, usi…………Mh! Rich: Mbona unahofu. Ongea…….. “you are free” (“uko huru”) Speak anything (ongea chochote) Rose: Sawa dear. Nina swali nataka nikuulize. (Wakati huo Rose alikuwa aking’atang’ata vidole vyake kwa aibu. Kisha aliendelea….)?….Richard! sasa ni miaka minane imepita tangu tuwe wapenzi. Kati yetu, sote tumekuwa na furaha isiyo mfano na inatufanya tufurahie mapenzi yetu (Alishusha pumzi)---A’h-m!........Napenda kufahamu mpenzi, lengo lako ni lipi juu ya mapenzi yetu? Kikubwa zaidi…………….A-mm! Basi Rich: Vipi tena? Wewe ongea usihofu chochote hapa. Hujanizoea tu miaka yote hii? Rose: Si hivyo Rich. Utanioa lini niwe mkeo wa ndoa mpenzi? Nahisi umri pia muda mwingi umepita hatulizungumzii hili! Samahani lakini. Rich: (alinyamaza kimya akimtazana Rose usoni kwa makini. Alishusha pumzi na kisha aliuliza swali baada ya Rose kumaliza kuongea kwake) Naomba tafadhali nieleze, nani kakutuma uniulize swali hilo? Tumeishi muda wote bila kuniuliza swali kama hilo. Vipi, unaweza kunieleza, ni nani amekutuma uniulize? Umepata bwana aliyekudanganya kukuoa nini? Haya niambie nijue nijikate ingali mapema sijachelewa.  Rose: Samahani Rich. Sikupanga iwe hivyo lakini……….Ah! Rich: Lakini nini? Sikiliza Rose, nakupenda sana zaidi ya unavyodhani. Lakini ninahitaji na wewe unijibu, uko tayari? Rose: Ndiyo Rich, please! (tafadhali) Rich: Ok!.....Sasa fahamu kuwa, sitakuoa wewe Rose. Unaweza kunieleza, kwa nini nikuoe wewe? Baada ya jibu pia swali lake Richard, Rose alibaki kimya akimkodolea macho huku akitokwa na machozi. Hakika furaha yake iligeuka uchungu mkali ulioiteka nafsi yake. Aliwaza na kuwazua mengi wakati huo. Aliwaza pengine ingekuwa sahihi kwake kumuadhibu Richard vikali. Kama si hivyo, alihisi pengine bora angejiua kuikwepa aibu. Upande mwingine wa nafsi yake ulimtaka avute subira pengine amjibu Richard swali lake kuwa kwa nini anastahili kuoana naye. Yote aliyatafakari akiwa mkimya na bumbuwazi lilimshika. Alitamka pasipo hiari yake kwa hasira kisha alinyanyuka. “SAWA! SAWA Rich! Hakika ngoja nikuonyeshe” Alinyanyuka na kutoka kitandani kwa jazba. Je, nini kilifuata kati yao?

Sample Read

3,000 Tsh.

Bei

KIU YA DAMU -FADHAA ni riwaya ambayo msuko wake ni wa kisimulizi. Riwaya hii inasimulia kisa cha kusisimua ambacho kiliikumba familia moja huko Bagamoyo. Kijana Mbununu anafumwa na kiu ya kuimwaga damu ya mkewe wa ndoa aliyekuwa mjamzito, kwa wivu wa mapenzi alihisi mkewe huligawa tunda lake la huba kwa jirani yake. Hisia za kisasi zinamfanya Mbununu kuua mfululizo kisha anajaribu kujiua ili kuukwepa mkono wa sheria. Kabla hajafanikiwa kujiua, Mbununu anaokolewa na jeshi la polisi kisha kupelekwa hospitalini ambako anapata tiba kisha kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma zilizomkabili. Jambo la kushangaza, Mbununu asiyejua kusoma wala kuandika, anaipoteza sauti yake kutokana na dawa zilizolikwangua koromeo lake. Je, mahakama ilichukua hatua gani kuujua ukweli wakati Mbununu hakuwa akijua kusoma wala kuandika, pia hakuwa na sauti tena ya kuweza kujieleza kwa kina? Soma ndani ya riwaya hii ujifunze jinsi mkasa huu unavyoweza kuyabadili maisha yako ya kila siku.

Sample Read