5,000 Tsh.

Bei

SIRI YA RAIS ni mfululizo wa riwaya inayoyaakisi maisha ya muuguzi, Tamali. Akiwa binti mbichi, maisha yake yanaingia mashakani. Mateso anayoyapata Tamali na mama yake yanatokana na siri nzito aliyoamua kuitunza kwa kuulinda wajihi wa baba yake kisiasa. Baba yake ambaye ni Rais Patrick Mzobe anachukua jukumu la kumkalia kooni bintiye ili asipate nafasi ya kuuanika uovu ambao taifa lilistahili kuujua. Je, ni siri gani Tamali anaificha na kuyafanya maisha yake yawe ya mashaka dhidi ya baba yake? Inaanza hivi…. KWA NINI? Kwa nini dunia ni onevu sana? Kwa nini ni sahaulifu? Si sahaulifu tu, bali haitendi haki kwa uonevu na kiburi. Haki ya kila mja mwenye pumzi na mapenzi ya kuishi vile atakavyo haipo duniani. Mwenye haki na kiu ya kuyafanya maisha yake yawe yake, peke yake pasipo vikwazo wala uonevu, akiwasaidia wengine kwa huba, hugeuka mhanga. Siwezi jua kwa undani. Siwezi amini kama kweli macho yangu ni makengeza, ubongo wangu umechoka kufikiri, hata sauti yangu haitoki nje ya jumba hili la mateso. Inawezekana, sauti yangu kufungiwa na mawazo yangu kuchacha kisha kuangamia ndani ya jumba hili la wahalifu? Je, ni makusudi ya aliye niumba. Tazama, ukuta mrefu umelizunguka jumba hili na kulinyima hewa ya kutosha. Tupo ndani ya shimo kama si pango la wanyonge. Mbali na kuta zake ndefu, senyenge yenye moto, imetanda kwa hila. Yote hayo asitokee mtoro, mtoro muuaji, mtoro mtoa roho. Najiuliza, je, mimi kweli ni muuaji? Hapana! Mie sijaua. Sijawahi kuua hata kuwaza kuutoa uhai wa kiumbe yeyote duniani kwa jeuri. Kazi yangu ni kuyafanya maisha ya kila kiumbe yastawi kama mche wa ua waridi kwenye udongo mzuri. Maisha ya kila kiumbe ni matamu awapo huru kuiona nuru, akitumbukizwa katikati ya giza la uvungu maisha yake huwa ya mashaka kama popo asiyeweza kujitafutia mchana. Nakumbuka kisha nasahau, sijui hapa nilifika lini na nitatoka lini. Nasikia mkisema kwa sauti za kunilaani, “Kaa mbali na Tamali katili, kwake kuua ni jambo rahisi kama kuubeba unyoya wa kuku.” Nawasikia lakini siwezi kuwajibu. Siwashangai wala siwapuuzi, hiyo ni nafasi yenu na uhuru wenu kwa sasa. Haya ni maisha yangu nisiyo yaota wala kuyawaza kuishi nayo tangu kuzaliwa kwangu. Ningali nikiendelea kuwaza, nimedhoofu mwili wangu, nipo hohehahe sijiwezi. Nunua na pakua riwaya hii uburudike na kuelimika…

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI RAGIN MMBAGA