8,000 Tsh.

Bei

Nilizaliwa tarehe 02/02/1978 katika kijiji cha ujamaa Nambalapala kilichopo Kata ya Kipara, Zone ya Mnero Mission, Tarafa ya Ruponda wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi. Mkoa huu ni maarufu sana kwa kupatikana kwa gesi asilia pia kulima zao la korosho, mandhari yake haitofautiani sana na visiwa vya Zanzbar. Wenyeji wengi wakiwa waumini wa dini ya kiislamu. Nikiwa ni mzaliwa wa pili kati ya watoto nane kwa wazazi wangu, mzee Abdalah Mohamed Musa Maigala na mama yangu kipenzi Asumin Hamisi. Wazazi wangu walikuwa wakulima huku wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama yalivyo maisha ya kijijini. Maisha hayakuwa mazuri sana na kutokana na kipato kidogo, hivyo tulilazimika kukomaa kimawazo tukiwa katika umri mdogo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Nilikuwa mdadisi sana kuhusiana na mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea katika familia yetu tangu nikiwa mtoto. Nakumbuka siku moja niliwauliza wazazi wangu namna ambavyo nilizaliwa mpaka nakua. Mama alishangazwa na swali langu akainamisha kichwa chake chini kisha akavuta pumzi na kusema; “Mwanangu Suleiman sasa umekua, nasema hivyo kwa sababu swali ulilouliza linaonyesha kuwa unataka kujitegemea kiakili” Baada ya kusema maneno hayo alivuta tena punzi na kunitazama huku akitokwa na machozi kisha akaendelea; “Wewe ni mtoto wangu wa pili. Ilikuwa usiku wa manane nilipoanza kuhisi uchungu, Baba yako alichukua baiskeli yake na kufunga tenga lake la kwendea shambani ili nikae humo. Mwanangu ilikuwa hakuna jinsi ya kupata usafiri mwingine kwa nyakati hizo za usiku. Nilipata taabu kubwa sana njiani kwa sababu tenga lile nililobebewa lililkuwa dogo hivyo kunipa wakati mgumu katika ukaaji.

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI AQRAM MWAKANSOPE