5,000 Tsh.

Bei

ALIPOCHEKA, alipendeza. Tabasamu lake zuri, tabasamu linaloshawishi na kubembeleza, huwafanya watu, hususan wanawake wamsogelee na kumsalimia. Baadhi ya wanawake hao husisimkwa miili pindi tu waisikiapo sauti yake na huchanganyikiwa pale wanaposhikana mikono. Pia, alikuwa na sauti ya kipekee, sauti iliyogusa hisia zao na kuamsha gharika la maraha kwenye michipuo ya fahamu zao. Ni kijana wa kiume, mwenye sura ya ucheshi na macho ya upole. Hakuwa mwoga wa kutazamana na mtu, lakini hakupenda kutazamana na mwanamume mwenzake. Kwake, macho ya mwanamume mwenzake yalikuwa na kitu asichokijua, kitu kisichopendeza. Yalimtisha! Hata hivyo, hali hiyo ilikuwa kwa wanaume tu, siyo kwa macho ya wanawake. Aliyapenda macho ya wanawake na ilipotokea akakutanisha macho na kiumbe yeyote wa kike, katu hakuyabandua macho yake. Ndani ya mboni za mwanamke yeyote kulikuwa na kitu fulani kisichoelezeka, lakini kilichomvutia na kumsisimua.

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI INNOCENT NDAYANSE

5,000 Tsh.

Bei

Kila mwanadamu aishiye chini ya jua hupenda kuishi maisha bora. Suala linakuja kuwa ni vipi atafanikiwa. Kila mmoja ana mbinu yake ya kutimiza ndoto yake kwa namna anayoona inafaa. Riwaya hii inagusa jamii tuliyonayo na iki chua yale yaliyotendeka miaka iliyopita na yanayoendelea kutendeka katika kipindi hiki. Songa nayo...

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Siyo kwamba kila mwanadamu anaamini kuwa ili utatute tatizo lolote linalokukabili lazima uwe na elimu ya kiwango kikubwa, uwe mjanja wa mjini au mcha mungu utegemeaye maombezi kwa kufanikisha mambo yako. Wapo ambao hawapo katika makundi yote hayo. Wao huamini zaidi katika kile kinachoitwa ‘nguvu za giza.’ Katika riwaya hii utashuhudia mambo yanayofanyika chini ya jua, yakiwastaajabisha wale wenye akili za kawaida na kuwasisimua wenye mioyo ya kijasiri.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa pesa ni zaidi ya kila kitu maishani. Ukiwa na pesa hakuna litakaloshindikana. Ni pesa hizo zinazoweza kuzua uhusiano mzuri kwa watu kama ambavyo pia zinavyoweza kusababisha maafa yasiyotarajiwa. Pesa ni sabuni ya roho na pia pesa huweza kuwa chachu ya matatizo. Katika riwaya hii ya aina yake, pesa zimedhihirisha jinsi zinavyoweza kuwa chanzo cha furaha maishani au kero na mtafuruku katika jamii. ni kipi kilichojiri? Fuatilia mkasa huu mzito wenye mchanganyiko wa mapenzi, visasi na mauaji ya kikatili...

Sample Read

8,000 Tsh.

Bei

Kamba Kiroboto yuko katika ulimwengu wa aina yake. Katika kipindi fulani maishani alijiona kuwa yu binadamu kamili, mwenye heshima mbele ya jamii, kwa watu wa marika yote. Halafu kikaja kipindi ambacho alijiona hatofautiani na mnyama. Akajenga chuki dhidi ya wanadamu wenzake, hata akakaribia kujenga chuki dhidi ya nafsi yake. Hali hiyo haikutokea kama muujiza, hapana. Kulikuwa na sababu maalum. Ndipo anapoweka nadhiri ambayo hakuwa tayari kuitengua kwa namna yoyote ile. Anaamua kufanya chochote kile, wakati wowote, mahali popote na dhidi ya mtu yeyote mlengwa. Huenda hicho atakachokifanya kikawa kizuri kwake lakini kikawa ni pigo zito kwa mwingine. Hata hivyo, hajali athari yoyote itakayotokea upande wa pili. Ana msimamo thabiti katika uamuzi wake. Kama atakuwa amevunja sheria ya nchi hilo ni jambo lingine, lakini ameamua. Uamuzi wake ndiyo kitu muhimu hata kama utekelezaji utaigharimu roho yake... anajiamini na anaamini kuwa uamuzi wake ni sahihi zaidi ya ushauri wa mwanadamu mwingine yeyote aliyezaliwa chini ya jua. Vitabu vingine vitakavyotoka hivi karibuni ni MILIONI THELATHINI, KARATA YA BARADHULI na GUBERI LA KIMANYEMA. Kitabu kingine ambacho kiko sokoni ni DOMO LA MAMBA.

Sample Read

6,000 Tsh.

Bei

Wakati niki kiria kuchapa kitabu cha riwaya hii, mmoja wa wasomaji wangu ambaye aliwahi kuisoma gazetini, aliniambia kuwa ilimvutia sana na hivyo, akawa akiisubiri kwa hamu. Hata hivyo, mchakato wa uchapaji ulikumbwa na matatizo yaliyosababisha kusitishwa kwa muda uchapaji. Zilipopita siku nyingi, msomaji huyo, Clara John aliniuliza ni kwa nini sijakichapa kitabu na aka kia hatua ya kuwa tayari kugharimia uchapaji huo. Nikiwa katika maendeleo ya kuufanyia marekebisho mswada huu, mara mawasiliano kati yangu na Clara John yalipotea. Nikajitahidi kutafuta kwa njia ya mtandao wa Facebook na WhatsApp, sikumpata. Simu yake pia ikawa haipatikani hewani. Ni baada ya takriban mwezi mmoja baada ya kupoteza mawasiliano ndipo nilipopata taarifa kuwa alifariki dunia gha a kwa presha akiwa huko mkoani Iringa. Ilikuwa ni taarifa iliyonisikitisha sana kwani tayari nilikuwa katika hatua za mwisho za kwenda kiwandani. Nguvu ziliniisha, nikajikuta nikikata tamaa na kutojisikia hamu tena ya kuuchapa mswada huu. Jambo lingine lililonichaganya ni kuhusu picha yake iliyokuwa imeandaliwa kama pambo la jalada, jambo alilolia ki. Sikuwa najisikia kuwa radhi kuitumia tena ilhali yeye mwenyewe hayupo duniani. Ingependeza kama angelikuwa hai, akishike kitabu chenye jalada lenye picha yake! Hata hivyo, baada ya kujadiliana na baadhi ya watu wake wa karibu, nikashauriwa niitumie tu picha yake katika kumuenzi. Tulimpenda Clara John, lakini Mungu alimpenda zaidi.

Sample Read

5,000 Tsh.

Bei

Kuandika riwaya ili ichapwe gazetini ni jambo moja. Kuandaa muswada wa riwaya kwa madhumuni ya kuchapwa kitabu ni jambo jingine. Domo la Mamba ni riwaya ambayo niliitumia katika gazeti moja na kupata simu nyingi zinazoulizia kitabu chake. Wengi niliwajibu. Baadhi yao waliridhika kwa majibu yangu, baadhi hawakuridhika. Niligundua kuwa wasomaji wengi hu kiri kuwa gharama za uchapaji kitabu hazizidi shilingi 500 kwa nakala moja. Mtu mmoja alidiriki kuniuliza: Shilingi laki tatu au nne hazitoshi kuchapa nakala elfu moja au mbili? Nilishangaa, nikakosa jibu! Gharama za uchapaji zimepanda maradufu. Ukitaka kuchapa kitabu chenye zaidi ya kurasa 100 itabidi ujipange na kujikamua mifuko na hasa kama unataka kitabu hicho kiwe kwenye ubora unaostahili. Isitoshe, linapokuja suala la kuandaa muswada inabidi baadhi ya mambo yafanyike, miongoni mwa yaliyo muhimu yakiwa ni uhariri na uhakiki. Haya nayo hugharimu pesa zisizo haba. Kitabu hiki nimekiandaa katika mazingira magumu lakini nikiwajali zaidi wasomaji wangu na jamii kwa jumla. Ni katika kipindi hicho ndipo nilipowagundua mara ki wa kweli, walioijua dhamira yangu huku pia wakitambua ka jinsi mtikisiko wa uchumi ulivyoniteteresha katika kuitimiza azma yangu. Ni mara ki hao ambao walikuwa nami bega kwa bega, wakiniunga mkono kwa hali na mali, tendo lililochangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uchapwaji wa kitabu hiki. Ninawashukuru sana ndugu na mara ki hao na zaidi, ninawashukuru wasomaji wangu ambao mara nyingi wamekuwa wakinihimiza kuchapa vitabu vya riwaya nilizotoa katika magazeti mbalimbali. Domo la Mamba ni mwanzo wa matoleo ya riwaya hizo. Nyingine ziko jikoni, zikiiva, zitapakuliwa na kutengwa mezani tayari kwa kuliwa. Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.

Sample Read