5,000 Tsh.

Bei

“Ina maana unafurahia kwa ushindi wake?” “Of course yes! Jamaa anapiga ngumi za kilo nyingi, yaani kamtwanga Kibwana mpaka kamwacha na meno ishirini na nane…” “Na uhai kamwondoa!” “What? Unasemaje wewe?” “Ndiyo maana nikakuuliza unafurahia ushindi wake?” Badala ya kujibu swali lile Stella aliamua kuinuka na kutoka nje ya ukumbi huo uliosheheni watu waliokuwa wakishangilia kwa kelele na mbinja zenye kukera masikioni mwa wasiopenda. Ijapokuwa alipata upinzani mwingi kwenye katikati ya mashabiki hao wa mchezo wa ngumi, mwishowe alifanikiwa kutoka kabisa na kujikuta nje. Baada ya kujikuta nje akagundua kuwa hana pa kwenda zaidi ya kusimama na kushangaa magari yapitayo kutoka Kurasini kwenda Shule ya Uhuru. “Stella! Stella!” sauti ya kiume ikasikika nyuma yake ikiita kwa mbisho. Stella hakugeuka nyuma zaidi ya kuikusanya mikono yake kifuani mwake na kutulia kimya kabisa. Mtu mzima, ambaye ngozi ya mashavu yake tayari ilianza kujikusanya na kufanya makwinyanzi alisimama kando ya binti huyo. Hakuwa mtu mzima bali msichana mwenye kadiri ya miaka ishirini na tano na thelathini hivi. “Sasa kilichokutoa nje ni nini?” kule mtu mzima akauliza. “Sasa si pambano limeisha, nikae nifanye nini?” Stella akajibu. “Sidhani kama umetoka kwa sababu hiyo!” Yule mtu mzima akaonesha shaka. “Mzee taksi, twende!” dereva wa taksi alimwita mzee huyo kwa sauti kwa kuwa yeye alikuwa upande wa pili wa barabara ile. Gari yake aina ya Volvo ilikuwa bado inaunguruma. “Tuondoke na hii….” Yule mtu mzima akamwambia Stella. Msichana huyo hakujibu zaidi ya kubetua mabega ‘sitaki’. “Tunapanda UDA, sasa hivi litakuja…” “Utapandaje UDA na mimi nipo? We ni malkia wangu watakiwa kutumia kebu mama kufika kwako…”

Sample Read

RIWAYA NYENGINE ZA MWANDISHI RICHARD AMATA